Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imenyakua ubingwa wa pili wa
Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN
baada ya kuibwaga Mali kwa magoli 3 kwa 0 kwenye fainali iliyopigwa Jumapili
kwenye uwanja wa Amahoro jijini Kigali nchini Rwanda.
Mchezaji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Meshack Elia aliifungia
timu yake mabao mawili kabla ya Jonathan Bolingi kupachika bao la tatu na
kuizamisha jahazi ya timu ya Mali.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ni nchi ya kwanza kulitwaa Kombe la
CHAN mwaka 2009 lilipoanzishwa na kuchezwa katika ardhi ya Ivory Coast ambapo
waliifunga Ghana kwa mabao 2 kwa 0 kwenye fainali.
Wakati huo huo Ivory Coast wameshika nafasi ya tatu katika michuano
hiyo ya CHAN 2016 kufuatia ushindi wa magoli 2 kwa 1 dhidi ya Guinea katika
mechi ya mapema iliyochezwa kwenye uwanja huo wa Amahoro, Kigali nchini Rwanda.
No comments:
Post a Comment