Wagosi
wa Kaya timu ya Coastal Union ya Tanga wamevunja mwiko wa AZAM FC kutokupoteza
mechi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa kwa bao 1 kwa
bila kwenye mechi iliyochezwa Jumapili kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Bao
hilo la Coastal Union lilifungwa na beki wa kulia wa timu hiyo Miraji Adam katika
dakika ya 67 ya mchezo kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya kupokea pasi fupi
kutoka kwa Adeyum Saleh Ahmed.
Adhabu hiyo ilitokana na golikipa wa AZAM FC Aishi Manula kuudaka mpira na kulala nao kwa muda mrefu akiwa anaugulia maumivu badala ya kuutoa nje na kuonyesha ishara ya kuomba msaada, mwamuzi wa kati wa mechi hiyo Vicent Mlabu kutoka Morogoro kuamuru adhabu hiyo ipigwe kuelekeo lango la AZAM FC.
Matokeo
hayo yameifanya Coastal Union kufikisha pointi 16 kwa mechi 19 walizocheza na
kuondoka katika nafasi ya kukalia mkia kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment