Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Wednesday, February 3, 2016

MWANANZILA:AKERWA NA SUALA LA MKOA WA TABORA KUSHIKA MKIA MATOKEOYA DARASA LA 7



LUDOVICK MWANANZILA
Na Allan Ntana, Tabora

MKOA wa Tabora umeshika nafasi ya mwisho katika matokeo ya wanafunzi
waliohitimu elimu ya msingi kwa mwaka  2015.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa huo Ludovick Mwana alipokuwa
akifungua kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi uliopo mjini Tabora.

Akionyesha kusikitishwa na matokeo hayo Mwananzila amesema
haiingii akilini mkoa huo kushika nafasi ya mwisho kati ya mikoa yote
26 ya Tanzania bara, pamoja na kuwepo mikakati ya kiutendaji wa kuongeza ufaulu unaongezeka iliyowekwa  kupitia kikao cha tarehe 29 Januari 2015.


‘Nilijiuliza maswali mengi sana baada ya kupata matokeo, kulikuwa na
sababu gani ya kuitisha mkutano wa wadau na kuweka maazimio lukuki kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na kuongeza ufaulu wa watoto wetu.’ Amesema kwa masikitiko.

Mwananzila amebainisha kuwa kitendo cha mkoa huo kufanya vibaya katika matokeo hayo kimechangiwa na halmashauri za mkoa huo kushindwa kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa katika vikao husika ikiwemo kutosimamia vizuri suala zima la elimu.

Aidha amesema uzembe na vitendo vya ulevi kwa baadhi ya walimu
vimechangia pia kufanya vibaya kwa watoto kwani muda mwingi wanautumia kwenye mambo yao binafsi ikiwemo biashara za bodaboda, ulevi na nyinginezo na sio kufundisha watoto darasani.

Akionyesha kuchukizwa na vitendo hivyo Mwananzila amewaagiza Wakurugenzi wa halmashauri zote kuwasilisha ofisini kwake majina ya walimu walevi wote sambamba na wale wanaojihusisha na biashara za aina yoyote ile kwani hao ndio chanzo kikubwa cha kurudisha nyuma maendeleo ya elimu.

Aidha amewaagiza Wakurugenzi hao kuwaandikia barua za onyo kali wakuu wa shule za msingi wote waliofaulisha watoto chini ya 10 huku
akiwataka pia kuwaondoa mara moja katika madarasa husika walimu wote waliofaulisha watoto chini ya 7.

Aidha amewataka Wakuu wote wa wilaya mkoani humo kusimamia maagizo hayo na kuhakikisha taarifa hizo zinamfikia ofisini kwake haraka
iwezekanavyo ili aweze kuchukua hatua stahiki kwa wahusika wote.
Mwananzila pia amewaagiza wakuu hao wa wilaya kufuatilia na kuwabaini maafisa wasiotoa taarifa za kiutendaji kwa wakati na pale zinapohitajika.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uyui Saidi Ntahondi ameshauri vikao vya wadau kufanyika mara mbili au zaidi kwa mwaka tofauti na sasa ambapo kinafanyika kikao kimoja tu kwa mwaka jambo linaloathiri ufuatiliaji wa maazimio ya vikao hivyo.

No comments: