![]() |
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS, TAMISEMI, GEORGE SIMBACHAWENE |
Aina ya Vikao na Nyakati za kufanyika
NA
|
AINA YA KIKAO
|
MUDA WA KUKUTANA
|
1.
|
Mkutano wa Wakazi wa Kitongoji.
|
-Hutakiwa kuketi kila mwezi mara moja
na wakati mwingine wowote kulingana na dharura.
-Kamati ya Kitongoji ni kwa
mfululizo huo tena kabla ya Mkutano wa Wakazi wote na wakati mwingine wowote
kulingana na
dharura
au mahitaji.
|
2.
|
Mkutano wa Wakazi wa Mtaa.
|
-Hupaswa kufanyika kila baada ya miezi 2
na kisha kulingana na dharura.
-Kamati ya mtaa ni kwa
mpangilio huo, kabla ya Mkutano wa Wakazi wa Mtaa.
|
3.
|
Mkutano Mkuu wa kijiji
|
Kila baada ya miezi 3 na pia kulingana na dharura.
|
4.
|
Halmashauri ya Kijiji
|
-Kila baada ya mwezi na kabla ya
mikutano Mikuu ya Kijiji na wakati mwingine kulingana na dharura.
|
5.
|
Kamati za
Kudumu za
Halmashauri ya Kijiji
|
-Kila mwezi na kabla ya Halmashauri
kuketi na wakati mwingine kulingana na dharura.
|
6.
|
Kamati za huduma mbalimbali
|
-Kuna kamati za huduma
katika Kijiji kama vile Kamati ya Shule,Kamati ya UKIMWI, Kamati ya
Mradi,n.k. ambazo hupaswa
kukutana kulingana na Sheria
au Mwongozo unaoanzisha kamati hiyo.
|
7.
|
Kamati ya Maendeleo ya Kata
|
-Hupaswa kukutana kila baada ya miezi
3 na wakati mwingine wowote kulingana na dharura.
|
8.
|
Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo
|
-Hupaswa kukutana kila miezi 3 mara
moja na kulingana na dharura.
|
9.
|
Kamati za
Kudumu za Mamlaka ya Mji Mdogo
|
-Kila baada ya miezi 3 na kulingana
na dharura isipokuwa ile kamati inayohusika na fedha ni kila mwezi.
|
10.
|
Mabaraza ya Madiwani
ya Wilaya,
Mji, Manispaa na Jiji
|
-Kila baada ya miezi 3 na kulingana na dharura.
|
11.
|
Kamati za
Huduma za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji
|
-Kila baada ya
miezi 3 na
kulingana na dharura isipokuwa ile inayohusika na fedha ni kila mwezi.
|
12.
|
Bodi /Kamati
za huduma katika
Halmashauri
|
-hukutana kwa mujibu wa
matakwa ya Sheria au miongozo inayoanzisha Bodi/Kamati hizo.
|
No comments:
Post a Comment