Na,Thomas
Murugwa,Tabora.
Afisa
mtendaji wa kijiji cha Igalula wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora Ramadhan
Athuman Msumeno amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuomba rushwa kinyume
cha sheria namba 11/2007 ya TAKUKURU.
Upande
wa mashitaka ukiongozwa na wakili Edson Mapala wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa TAKUKURU umedai mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa
Agatha Chigulu kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe 9 Disemba,2015.
Wakili
Mapalala alisema kuwa siku hiyo afisa mtendaji huyo aliomba shilingi laki tatu
(300,000/-) toka kwa Dotto Joseph ili asimchukulie hatua za
kisheria.
Mapalala
ameongeza kuwa mtuhumiwa akiwa ni mtumishi wa serikali katika halmashauri ya
wilaya ya Sikonge aliomba fedha hizo ili asimchukulie hatua kutokana na tuhuma
za kumuua mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Regina Daud.
Mtuhumiwa amekana shitaka hilo na amepelekwa
rumande baada ya kukosa wadhamini wenye sifa hadi tarehe 23 mwezi huu kesi hiyo
itakapoanza usikilizwaji wa awali.
No comments:
Post a Comment