Na Ramadhan Faraji, Tabora.
Ligi daraja la kwanza imeendelea Jumapili kwenye
uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Rhino Rangers waliikaribisha
Mbao FC ya jijini Mwanza.
Katika kipindi cha Kwanza timu hizo zilicheza kwa
kusomana na kushambuliana kwa zamu na zilimaliza dakika 45 za kipindi hicho
bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Mbao FC
ya jijini Mwanza ilifanyikiwa kupachika magoli 2 na wenyeji Rhino Rangers
wakiambulia goli 1.
Hadi dakika 90 zinakamilika Mbao FC waliibuka na
ushindi wa Mabao 2 kwa 1 la Rhino Rangers.
Usukani wa Ligi hiyo kwa kundi C unaongozwa na
Timu ya Polisi Tabora yenye pointi 27 sawa na Geita Gold Mine yenye pointi 27
ila zikitofautiana magoli ya kufanga na kufungwa.
Timu za kundi C ligi daraja la kwanza zimebakisha
mechi moja kila timu kukamilisha mzunguko wa pili ambao utaamua timu ipi ipande
daraja na kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao.
Kwa vinara wa kundi hilo Polisi Tabora
watakamilisha mzunguko huo kwa kuikaribisha JKT Orjolo na Geita Gold Mine
itakutana na JKT Kanembwa.
Kila la heri kwa Polisi Tabora kucheza ligi kuu
msimu ujao.
No comments:
Post a Comment