Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Monday, February 1, 2016

WAKAZI WA WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII, CHF.



Na Hastin Liumba,Uyui
 
Mkuu wa wilaya ya Uyui mkoani Tabora Zuhura Mustapha Ali imewataka wakazi wa wilaya hiyo kujiunga mfuko na wa afya ya Jamii (CHF) ili waweze kunufaika na matibabu kwa gharama nafuu na kwa uhakika.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii CHF uliofanyika katika kata ya Mabama wilayani humo.

Amesema licha ya wilaya hiyo kufanya vizuri kwa wakazi wake kuchangia na kujiunga kwenye Mfuko  huo bado iko haja  ya kuendelea kuwahimiza wale ambao hawajajiunga wafanye hivyo na kisha kunufaika.

Zuhura amesema wilaya ya Uyui kwa sasa imefikia asilimia 24.7 ya wakazi wake kujiunga na Mfuko huo wa Afya ya Jamii na kuifanya kuwa wilaya ya 10 kitaifa.

Meneja wa mfuko wa taifa wa Bima ya Afya kanda ya Magharibi (NHIF)
Emmanuel Adina amesema afya ni jambo jema kwa kila mwanadamu hivyo wakazi wa wilaya ya Uyui watumie fursa hiyo kujiunga na CHF.

Aidha  ametumia fursa hiyo kulipia wananchi watano kiasi ha Tsh.
5,000  kiwango kilichopangwa kwa ajili ya siku hiyo uzinduzi kwa lengo la kuwafikia  wazee wasiojiweza pamoja na wajane wasio na uwezo.

Naye Meneja kiongozi na rasilimali watu wa (NHIF) toka makao makuu ya mfuko huo Grace Kalanje Lobulu amesisitiza wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za afya.

Lobulu amesema suala la kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF iwe ni ajenda ya kudumu kwa viongozi wa wilaya hiyo.


No comments: