Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, February 14, 2016

KOMBE LA SHIRIKISHO: MAAFANDE WA JWTZ RHINO RANGERS USO KWA USO NA MWADUI FC



Na Ramadhan Faraji, Tabora.

Rhino Rangers yenye masikani yake mjini Tabora itapimana ubavu na watoto Julio Mwadui FC kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Maarufu kama Azam Sports Federation Cup itakayoanza kutimua vumbi tarehe 26 mwezi huu.

Mechi hiyo itapigwa tarehe 27 mwezi huu ambapo Rhino Rangers watabeba vifaa vyao vya kivita kuifuata Mwadui FC nyumbani kwao Shinyanga.

Maafande hao wa Rhino Rangers wanakila sababu ya kuzikonga nyoyo za mashabiki wake baada ya timu hiyo kutofanya vizuri kwenye ligi daraja la kwanza iliyomalizika mwishoni mwa wiki.

RATIBA YA MECHI NYINGINE NI KAMA IFUATAVYO

Februari 26, 2016
Ndanda FC Vs JKT Ruvu (Nangwanda, Mtwara) 
Coastal Union Vs Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga)
Februari 27, 2016.
Mwadui FC Vs Rhino Rangers (Mwadui, Shinyanga)
Prisons Vs Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
Februari 28, 2016
Simba SC Vs Singida United (Taifa, Dar es Salaam) 
Panone FC Vs Azam FC (Ushirika, Moshi)
Toto African Vs Geita Gold (Kirumba, Mwanza)
Machi 1, 2016
Yanga SC Vs JKT Mlale (Taifa, Dar es Salaam)

No comments: