Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Thursday, February 11, 2016

JELA KWA KUUA BILA KUKUSUDIA





Na, Thomas Murugwa, Tabora.

 Mahakama kuu kanda ya Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka sita jela Diwani Lupepe mkazi wa Sikonge baada ya kumuona anahatia pamoja na kukuri kosa dogo la kuua bila kukusudia.

Adhabu hiyo imetolewa hivi karibuni na jaji Julius Malaba baada ya kumtia hatiani mshitakiwa kutokana na kitendo chake cha kukubali kosa dhidi yake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini.

Jaji Malaba amesema ametoa adhabu hiyo kwa  kuzingatia hoja zilizowakilishwa na  wakili wa utetezi Stella Nyaki kwamba mshitakiwa hakuisumbua mahakama kutokana na kitendo chake cha kukiri kosa hilo huku akijutia tendo alilofanya.

Wakili Nyaki aliiomba mahakama itoe adhabu ndogo kwa mshitakiwa kwa vile katika kipindi alichokaa mahabusu amejifunza mengi amejirekebisha, ana watoto wanne wanaomtegemea,hakuipotezea mahakama muda na pia ni kosa la kwanza.

Katika shauri hilo  wakili wa serikali Deusdedit Rwegire aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshitakiwa kwa kitendo chake cha kumuua mtu asiyekuwa na hatia.

Awali wakili huyo wa serikali aliiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo desemba 24/2013 katika kijiji cha kikungulu wilaya ya sikonge.

Wakili Rwegire alisema kuwa siku hiyo mshitakiwa akiwa amelewa bila kukusudia alisababaisha kifo cha Mbogo Masanja  kwa kumchoma tumboni kwa kutumia fimbo na kusababisha avuje damu nyingi.

Taarifa ya daktari inaonyesha kuwa Masanja ambaye sasa ni marehemu alifariki tarehe 30 Disemba 2013 kutokana na damu nyingi kuvujia tumboni.

No comments: