Na,
Thomas Murugwa, Tabora.
Mahakama
kuu kanda ya Tabora imetupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa
Ubunge wa jimbo la Tabora mjini lililofunguliwa na wanachama wanne wa Chama Cha
Wananchi CUF na kuwataka walipe gharama walizoingia wadaiwa.
Uamuzi
huo umefikiwa na jaji Leila Mgonya baada ya kukubaliana na pingamizi la mawakili
wa wadaiwa ambao ni mbunge wa jimbo, Msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria
mkuu wa serikali kwamba walalamikaji hawakuwa na mamlaka na pia hawakuonyesha
haki yao iliyovunjwa wakati wa zoezi la uchaguzi.
Jaji
Mgonya katika uamuzi wake aliousoma kwa saa mbili amesema kuwa anakubaliana
kwamba haki yao ya kuleta shauri hilo inatokana na kifungu namba 111 (1) cha Sheria
ya uchaguzi lakini hawakuwa na mamlaka kisheria.
“kutokana
na sheria za nchi ili mtu awe na mamlaka ya kufungua shauri la kupinga matokeo
kama siyo mgombea inabidi aeleze jinsi gani haki yake ilivyovunjwa na pia
alivyoumizwa” amesema jaji Mgonya.
Katika
maamuzi hayo, jaji Mgonya amewataka walalamikaji ambao ni wananchama wanne wa
CUF walipe gharama walizotumia wajibu maombi wakati wa uendeshaji wa
shauri hilo tangu lilipofunguliwa tarehe 25 Novemba 2015 hadi lilipomalizika.
Wanachama
hao wanne wa CUf ambao ni Jumanne Mtunda ,Johari Kasanga, Shaban Mussa na
Thomas Ayengo kupitia kwa wakili wao Job Kerario waliiomba mahakama itengue
matokeo ya uchaguzi uliompa ubunge Emanuel Mwakasaka wa CCM kwa madai haukuwa
huru na wa haki.
Upande
wa wajibu maombi ulikuwa unawakilishwa na wakili mwandamizi wa serikali Juma
Masanja pamoja na Kamaliza Kayaga aliyekuwa anamwakilisha mbunge wa jimbo hilo,Emmanuel
Mwakasaka.