Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Wednesday, March 30, 2016

YANGA, AZAM FC UWANJANI ROBO FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO



Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inaendelea tena Alhamis ya Tarehe 31 Machi, 2016 ambapo Yanga wataikaribisha Ndanda FC kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku Azam FC wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini humo.

Robo fainali ya kwanza ilichezwa tarehe 26 Machi, 2016 ambapo Geita Gold walikuwa wenyeji wa Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.Mwadui FC ilikuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Geita Gold kwa magoli 3 kwa 0.

Mechi ya mwisho ya robo fainali itachezwa tarehe 6 April,2016 ambapo Simba itacheza dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Droo ya nusu fainali ya kombe hilo itachezeshwa na kupangwa tarehe 7 April,2016.

Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu, ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) 2017.

No comments: