Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, March 13, 2016

LIGI DARAJA LA TATU:WATOTO WA MJINI TABORA FC WAWAFUNGA PINGU MAAFANDE WA JKT MSANGE




Mchezo wa kukamilisha ratiba ya mechi za Kundi B ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Tabora imepigwa kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi jioni ya Jumapili.

Mechi hiyo iliyotawaliwa na ufundi iliikutanisha miamba ya kundi hilo watoto wa mjini Tabora FC na wafunga buti JKT Msange zote za Manispaa ya Tabora.

Tabora FC waliwafunga pingu maafande hao wa JKT Msange baada ya kuwalaza kwa bao 1 kwa sifuri.

Ushindi huo umeifanya Tabora FC kuongoza kundi hilo kwa kufikisha pointi 14 na kuwaacha wapinzani wao wa karibu JKT Msange wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 13.

No comments: