Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Tuesday, March 1, 2016

WAUGUZI SITA WASIMAMISHWA KAZI HOSPITALI YA TEMEKE, DAR ES SALAAM



Dkt. KIGWANGALA
Na Cathrine Sungura, Dar es Salaam.

Wauguzi sita wa wodi ya akinamama wajawazito wa hospitali  ya rufaa ya Temeke,wamesimamishwa kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yao wakati wa kuwahudumia akinamama wanaofika kujifungua kwenye hospitali hiyo.

 Hatua hiyo imefikiwa kwenye ziara iliyofanywa hospitalini hapo na naibu waziri wa wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangwala.

Aidha,wauguzi hao wanatakiwa kifikishwa kwenye baraza la wauguzi na wakunga kwa kukosa uadilifu wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Waliosimamishwa kazi ni pamoja na Beatrice Temba, Marian Mohamed, Hadija Salum, Elizabeth Mwilawa, Agnes Mwapashe na Merion Said.

Hata hivyo Dkt. Kigwangwala ametoa siku 30 kwa manispaa ya Temeke kukamilisha chumba cha upasuaji cha akina mama wajawazito,miezi sita kwa vyumba viwili vya upasuaji  kuvifanyia ukarabati mkubwa na kuwa katika ubora unaotakiwa,miezi mitatu kwa  chumba  cha watoto wachanga kwa kuongeza vitanda 25 hadi 30  kutoka vitanda 9 vya awali ili kuepusha magonjwa ya kuambukiza.

No comments: