Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Monday, March 28, 2016

MCHUNGAJI LUTENGANO: "WATANZANIA TUMUUNGE MKONO RAIS MAGUFULI"

Na Allan Ntana, Tabora.

WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono jitihada zote zinazofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwa ameonyesha dhamira ya dhati ya kuiletea maendeleo makubwa nchi yetu.

Wito huo umetolewa na mchungaji Lutengano Asajile Mwasongela wa kanisa la TAG- Maranatha lililopo mtaa wa Cheyo B katika manispaa ya Tabora wakati wa mahojiano maalum katika kongamano la wanafunzi waliookoka lililofanyika Jumamosi katika ukumbi wa shule ya sekondari New Era.

Amesema heshima ya nchi imeanza kurudi, mwelekeo wa kiuchumi umeanza kuonekana, wabadhirifu wa mali za umma na wote wanaotumia madaraka vibaya wameanza kushughulikiwa ipasavyo ikiwemo kutumbuliwa majipu hali inayorejesha nidhamu ya kazi.

Mchunguji huyo amesema, “Sasa naionaTanzania mpya, makusanyo ya kodi yameanza kuonekana kwa kasi, kila taasisi ya serikali sasa inawajibika ipasavyo, uwajibikaji na nidhamu ya watumishi wa umma kwa wananchi imeanza kurudi, kwa kweli Rais anastahili pongezi.”

Amebainisha kuwa kasi ya utendaji wa Rais Magufuli inasifika ndani na
nje ya nchi na hata katika mitandao ya kijamii ya kitaifa na kimataifa
utakuta mijadala mingi inayogusa moja kwa moja kazi nzuri inayofanywa
na rais wetu.

Mchungaji Lutengano amefafanua, “Naomba sana Watanzania wote tumuunge mkono kwani ameifanya nchi yetu kuwa mfano wa kuigwa na viongozi wa mataifa mengine hapa duniani, lakini pia amedhihirisha wazi kuwa yeye ni Rais wa watu wote na hajali itikadi za vyama.”

Aidha amepongeza hatua iliyochukuliwa na Waziri wa Elimu Prof. Joyce
Ndalichako ya kurudisha mfumo wa zamani wa divisheni mashuleni kwani
unarahishaji hata upangaji madaraja kwa wanafunzi.

Mchungaji Lutengano amemuomba Rais Magufuli kupitia Waziri huyo kuzikarabati shule zote kongwe hapa nchini ili zirudi katika kiwango chake cha zamani kwa kuwa zimechakaa sana. 

Amezitaja baadhi ya shule hizo kuwa ni Tabora Girls’,Tabora Boys, Kazima, Milambo, Loleza, Ilboru, Moshi Tech, Ifunda na nyinginezo.

No comments: