Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, March 13, 2016

YANGA YAWATIA MBARONI MAAFANDE WA APR, YAWEZA KUKUTANA NA AL AHLY YA MISRI KATIKA MZUNGUKO WA PILI



YANGA WAKISHANGILIA BAO
Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga Jumamosi wameifunga APR ya Rwanda kwa Mabao 2 kwa 1 katika mechi ya mkondo wa kwanza wa mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi ya Mabingwa barani Afrika iliyochezwa kwenye uwanja wa Amahoro jijini Kigali nchini Rwanda.


Yanga walichukua dakika 20 za mchezo kuandika bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Juma Abdul aliiyeachia shuti kali nje ya kumi na nane ambalo lilimshinda golikipa APR Olivier Kwizera na kujaa nyavuni.

Hadi mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao moja kwa bila, katika kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo APR ilimtoa Djihad Bizimana na kumuingiza Janvier Benedata, Yanga ilimuingiza Simon Msuva badala ya Amissi Tambwe.

Katika kipindi cha pili APR ilifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Yanga kunako dakika ya 65 kona iliyochongwa na Patrick Sibomana ilipanguliwa na golikipa wa Yanga Mustapha kabla ya Nkizingabo kuupiga tena mpira uliookolewa.

Kunako dakika ya 71 Yanga wakawaadhibu wanajeshi hao wa APR kwa kupachika bao la pili kupitia kwa Thaban Kamusoko.

Kocha wa Yanga Hans Der Pluijm alifanya mabadiliko kwa kumtoa Haruna Niyonzima na kumuingiza mlinzi wa zamani wa APR Mbuyu Twite, ambapo APR ilimuingiza Ismael Nshutiyamagara badala ya Michel Rusheshangoga.

Wanajeshi wa APR hawakukata tamaa walizidi kufanya mashambulizi na kunako dakika ya 93 Patrick Sibomana akaipatia bao la kufutia machozi.
Hadi mwisho wa mchezo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1.

Timu hizo zitarudiana tena Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na mshindi kati yao atakutana na mshindi wa mechi ya Mabingwa wa Misri Al Ahly na Recreativo do Libolo ya Angola katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo ya Mabingwa barani Afrika.

Katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa nchini Angola Recreativo do Libolo ilitoka bila kufungana na Al Ahly.

Kwa matokeo hayo ya ugenini Al Ahly wanayonafasi kubwa ya kusonga mbele kwa kuwa watakuwa wakicheza nyumbani katika mechi ya mkondo wa pili.

Yanga ya Tanzania kama itaiondosha APR kuna uwezekano wa kukutana na Al Ahly ya Misri katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.


MATOKEO YA LIGI YA MABINGWA BARANI AFRIKA ( CAF CHAMPIONS LEAGUE) 

JUMAMOSI 12 MACHI, 2016
1.
Wydad Athletic Club

5-1

CNaPS Sport
2.
Mamelodi Sundowns

2-0

AC Leopards
3.
Kaizer Chiefs

0-1

Asec Mimosas
4.
Stade Malien

2-0

Coton Sport FC
5.
Club Africain

1-0

MO Béjaïa
6.
Recreativo do Libolo

0-0

Al Ahly
7.
APR FC

1-2

Young Africans
8.
Ahly Tripoli

1-0

El Hilal
9.
Zesco United

4-1

Horoya A.C
JUMAPILI 13 MACHI,2016
1.
US Douala
0-1
Zamalek 
2.
AS Vita Club
1-0
Clube Ferroviário de Maputo
3.
Etoile du Congo
1-1
ES Setif
4.
Warri Wolves
0-1
El Merreikh
5.
Olympique Khouribga
1-1
ES Sahel
6.
St. George
2-2
TP Mazembe
7.
Enyimba
5-1
Vital'O FC

No comments: