Na Halima
Ikunji,Kaliua
Wajumbe 20 wa halmashauri za
serikali za vijiji wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambao walikuwa wakinufaika na
fedha za mpango wa kunusuru kaya masikini unaosimamiwa na TASAF awamu ya tatu
wameondolewa kwenye mpango huo.
Akizungumza na waandishi wa habari
afisa mtendaji wa kata ya Ichemba wilayani humo Bryson Kikabiha amesema wajumbe
hao waliingia kimakosa kwenye mpango huo kwa kuwa walikuwa kwenye timu za
kutambua kaya masikini.
Amebainisha kuwa hatua hiyo
imesababishwa na uzembe wa makusudi uliofanywa wakati wa zoezi la kutambua kaya
masikini kwa kuwa wajumbe hao wa serikali za vijiji walikuwa na dhamana hiyo.
Akizungumzia suala hilo mmoja wa wajumbe
hao Gerad Katanga amesema kuwa waliamua
kuingia kwenye mpango huo wa kunusuru kaya masikini kutokana na wao kutolipwa posho
kwa nyadhifa walizonazo na hivyo kuwawia vigumu kujikimu kimaisha na familia
zao.
Mratibu wa TASAF awamu ya tatu wilaya
ya Kaliua Sabala Rukonda amesema kuwa wajumbe hao kama wataona hawakutendewa
haki wakate rufaa au wajiuzulu nyadhifa zao wafanye shughuli nyingine.
No comments:
Post a Comment