Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, March 6, 2016

WATUMISHI WAZEMBE WILAYANI NZEGA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU


NA Hastin Liumba.Nzega.

WATUMISHI wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora watakao
endelea kufanya kazi kwa mazoea na kushindwa kuwajibika katika nafasi
zao watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kusimamishwa kazi
kupisha uchunguzi.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha  Bajeti
ya 2016/2017 mkuu wa wilaya ya Nzega Jackline Liana  amesema hatosita
kuchukua hatua kali kwa mtumishi atakaye shindwa kwenda na kasi ya
serikali ya awamu ya Tano.

Amesema baadhi  ya watumishi wamekuwa na visingizio vingi ambavyo
havina msingi na kusababisha kukwamisha shughuli za maendeleo ya
wananchi na kuongeza kuwa mtumishi yeyote atakaye kuwa na tatizo la
kiutendaji anaweza kumsaidia.

Mkuu huyo wa wilaya amesema wananchi wanaimani na serikali iliyopo madarakani hivyo watumishi kwa kushirikiana na madiwani wanapaswa kuwa kitu kimoja ilikuhakikisha wanafanya kazi na kuleta maendeleo chanya kwa wananchi.

Akisoma mapendekezo ya Bajeti ya mwaka 2016/2017 Mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri hiyo Abraham  Mndeme amesema Halmashauri hiyo
inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni
54,227,902,489.

Amesema mapato ya ndani ni zaidi ya bilioni  1.6 matumizi ya kawaida
ni zaidi ya milioni 647.1  huku  mchango wa asilimia 60 kwenye
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni zaidi ya milioni 970.7.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Marco Kiwele amesema Bajeti hiyo
imelenga kuimarisha miundombinu ya barabara ya wilaya ya Nzega na
kutatua changamoto ya madawati katika shule za sekondari na msingi.

Akizungumzia utendaji wa wa watumishi mwenyekiti huyo aliwataka
watumishi ambao hawawezi kwenda na kasi ya maendeleo wanapaswa kutoa taarifa mapema ilihatua nyingine ziweze kuchukuliwa.

Wakati huo huo Halmashauri ya mji wa Nzega imepitisha mapendekezo ya
Bajeti ya mwaka 2016/2017 zaidi  ya bilioni 22.8 makisio hayo ni zaidi
ya asilimia 25 ya bajeti ya mwaka wa fedha uliopita.

Kati  ya fedha hizo bilioni  21 .6 ni ruzuku kutoka serikali
kuu,bilioni 1.1 ni fedha za makusanyo ya ndani ya Halmashauri.

No comments: