Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Friday, April 1, 2016

RADI YAUA MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA



Na Paul Christian, Tabora.

Mwanafunzi wa kike wa darasa la kwanza shule ya msingi Kakurungu kata ya Milambo Itobo wilayani Nzega Asia Paulo amefariki dunia baada ya kupigwa na radi.

Akizungumza na waandishi wa habari mtendaji wa kata ya Milambo Itobo Raphael Bundala amesema tukio hilo limetokea Alhamis mchana katika familia ya Ngelengi Makala katika kitongoji cha Mtakuja kijiji cha Kakurungu katani humo.

Amesema wakati wa majira hayo ya mchana ilinyesha mvua ya wastani iliyoambatana na radi ilipiga kwenye jiko la familia  hiyo na kusababisha kifo cha mwanafunzi huyo na kujeruhi watu wengine wanne. 

Raphael amewataja watu waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Hadija Juma mwenye umri wa miaka 40 amejeruhiwa ubavuni na sehemu ya paja, Sophia Ngelengi mwenye miaka 25 amejeruhiwa mbavuni,Salima Rashid mwenye miaka 21 amejeruhiwa kwenye paji la uso na mtoto wa miaka 6 Abdalla Ramadhan alipata majeraha miguuni.

Mtendaji huyo amefafanua kuwa majeruhi wote walitibiwa katika zahanati ya Kakurungu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

No comments: