Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, March 13, 2016

VPL: SIMBA SC YAJIKITA KILELENI KWA KUICHEZESHA GWARIDE TANZANIA PRISONS



Simba SC ya jijini Dar es Salaam imeendelea kujikita kileleni mwa ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa bila dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mechi iliyochezwa uwanja wa Taifa wa jijini Dar es Salaam, Jumapili jioni.

Bao pekee la wekundu hao wa Msimbazi lilipatikana dakika ya 87 ya mchezo kupitia kwa kiungo wake Awadh Juma Issa kufuatia kuachia shuti umbali wa mita 20 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Jonas Gerald Mkude.

Awadh alifanyikiwa kufunga goli hilo akitokea benchi na kuchukua nafasi ya Mzimbabwe Justice Majabvi katika dakika ya 70 ya mchezo.

Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha pointi 54 huku ikiwa imecheza mechi 23, wakiwaacha nyuma mabingwa watetezi Yanga kwa tofauti ya pointi 4 ambayo inakalia nafasi ya pili ikiwa na pointi 50 kwa michezo 21.Nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo inashikiliwa na Azam FC yenye pointi 47 kwa michezo 20 iliyocheza.

Katika mechi nyingine za ligi hiyo Mgambo JKT imeshindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani wa Mkwakwani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1 kwa 1 na Mwadui FC ya Shinyanga.


MATOKEO YA LIGI KUU YA TANZANIA BARA (VPL)

JUMAPILI 13 MACHI, 2016
1.
1-0
2.
4-0
3.
1-0
4.
1-1
 


 


No comments: