MBUNGE
wa jimbo la Nzega mjini mkoani Tabora, Hussein Bashe amesema alianza kuwa na ndoto za kuwa
mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 1994 akiwa anasoma sekondari.
Bashe
ametoa kauli hiyo Jumanne jioni alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha
Televisheni hapa nchini.
Amesema
kwa mara ya kwanza alijitosa kwenye kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi CCM mwaka
2005 ili kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi
ya chama hicho.
“Wagombea
wenye umri mdogo wakati huo tulikuwa mimi na Hamis Kigwangalla ambapo mwenzetu
Lucas Selelii alishinda na chama kumteua kugombea ubunge katika jimbo la Nzega.”amesema
Bashe.
Mbunge
huyo amefafanua kuwa mwaka 2010 aliingia tena katika kinyang’anyiro cha kuusaka
ubunge wa jimbo hilo akiwa pamoja na Hamis Kigwangalla na Lucas Selelii pamoja
na wagombea wengine ambapo yeye aliongoza kura za maoni za CCM akifuatiwa na
Lucas Seleli na Hamis Kigwangalla akawa wa tatu.
“Licha
ya kuongoza kura za maoni chama chetu kilimteua Hamis Kigwangalla kugombea
ubunge katika jimbo la Nzega na sisi tukamuunga mkono.”Amebainisha.
Bashe
amefafanua kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo la Nzega liligawanywa na
kutoa majimbo mawili ya Nzega mjini na Nzega vijijini.
“Nilikutana
na Hamis Kigwangalla na tukaamua kuweka tofauti zetu pembeni kisha tukakubaliana
mimi nigombee Nzega mjini na yeye agombee Nzega vijijini.”Amesema mbunge huyo.
No comments:
Post a Comment