Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, March 6, 2016

SIMBA YASIMAMA KILELENI MWA LIGI KUU TANZANIA BARA



Ibrahim Ajib wa Simba (kushoto) akimtoka beki wa Mbeya City, Haruna Shamte
Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imejikita kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuibika na ushindi wa mabao 2 kwa bila dhidi ya Mbeya City katika mechi iliyochezwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini humo.

Iliwachukua hadi kipindi cha pili cha mchezo huo, wekundu hao wa Msimbazi kujipatia bao la kwanza na la pili kupitia kwa wachezaji wake Danny Lyanga na Ibrahim Ajib kunako dakika za 75 na 90.

Ushindi huo umeifanya Klabu hiyo kufikisha pointi 48 ikiizidi Yanga inayokalia nafasi ya pili ikiwa  na pointi 47 sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kocha wa Simba Jackson Mayanja amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa kuendelea kuisapoti timu yao na pia amewapongeza wachezaji wake kwa kuifunga Mbeya City kwa mara ya kwanza katika uwanja huo wa Taifa.

Kwa upande wa kocha wa Mbeya City Kinnah Phiri amesema vijana wake walicheza vizuri, walichokosa ni bahati ya kufunga magoli kwenye lango la wapinzani wao.

No comments: