Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, March 6, 2016

MKUU WA MKOA WA TABORA ACHANGISHA MADAWATI 406,000 KATIKA HARAMBEE MAALUMU


LUDOVICK MWANANZILA

Sada Mohamed na Allan Ntana, Tabora

MKOA wa Tabora umeendesha harambee maalumu ya uchangiaji madawati ili kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli linaloelekeza kila wanafunzi nchini  kukaa kwenye dawati ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Katika harambee hiyo iliyoendeshwa na Mkuu wa Mkoa huo Ludovick Mwananzila fedha taslimu zilizokusanywa ni kiasi cha Tsh 3,975,000, ahadi za wadau Tsh. 43,700,000, madawati yaliyoahidiwa 406,000 na mchango kutoka Ofisi ya Rais TAMISEM ni kiasi cha sh 3,688,000.

Wadau waliotia fora katika harambee hiyo ni pamoja na mbunge wa jimbo la Tabora Kaskazini Almas Maige aliyetoa mchango wa Tsh. milioni 10, huku wabunge wengine wote wa mkoa huo wakichangia Tsh. milioni 1 kila mmoja akiwemo na Maige mwenyewe.

Katika harambee hiyo Mkuu huyo wa mkoa amewataka wadau hao kutekeleza ahadi zao haraka iwezekanavyo kwa kuwa shughuli ya ukusanyaji madawati au fedha za kununulia inatakiwa kukamilika ndani ya mwezi huu na mwezi ujao.

Awali akitoa taarifa kabla ya kuanza kwa harambee hiyo Mwananzila amesema mkoa huo una jumla ya shule za msingi za serikali 767 zenye jumla ya wanafunzi 427,353 wavulana wakiwa 214,495 na wasichana 212,858 na shule za sekondari za umma zikiwa 153 zenye jumla ya wanafunzi 50,406, wavulana 27,344 na wasichana 23,062 .

Amesema mkoa huo unahitaji jumla ya madawati 101,483 ambayo gharama yake ni takribani Tsh bilioni 11 ambapo kwa shule za msingi yanahitaji madawati 95,144  yaliyopo ni 88,000 na kwa upande wa
shule za sekondari yanahitaji madawati 6,339  yaliyopo ni 38,459.

Mwananzila amewataka wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri, makatibu tawala wa wilaya, Maofisa mipango na wengineo katika ngazi ya wilaya kushirikiana na kuhakikisha zoezi la ukusanyaji madawati linatekelezwa katika wilaya zao ili kufanikisha lengo hilo katika shule zote za mkoa huo.

No comments: