TUMBAKU |
MKUTANO MKUU WA “23” WA MWAKA WA WETCU LTD ULIOFANYIKA TAREHE 28
NA 29 MWAKA 2016 KWENYE UKUMBI WA MIKUTANO WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TABORA
TPSC.
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Chama Kikuu Cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi WETCU
LTD ambao kimsingi ni wawakilishi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa wakulima
wa Tumbaku (AMCOS) walijadili na kuhoji Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya WETCU
LTD kuhusu utekelezaji wa shughuli za Ushirika kwa mwaka 2015/2016 katika
maeneo yafuatayo:-
1) Ununuzi wa Gari jipya aina ya
ZX-V8 kwa thamani ya shilingi milioni 269,010,000/-,wakati
katika Mkutano Mkuu wa 22 wa mwaka 2015 wa WETCU LTD uliofanyika tarehe 01 na
02 April,2015 ulipitisha bajeti ya shilingi milioni 40 (40,000,000/-) kwa ajili ya ununuzi wa Gari.
Hoja zilizoibuliwa na Wajumbe wa Mkutano huo:-
ü Bodi ilipata wapi mamlaka ya kutumia
kiasi hicho cha fedha kununulia gari wakati wao walipitisha milioni 40.
ü Je kulikuwa na ulazima wa kununua
Gari hilo wakati baadhi ya vyama vya msingi vinakabiliwa na madeni na
havikopesheki.
ü Je, ni kwa nini fedha hizo (Tsh. 269,010,000/-) zisingetumika kulipa madeni ambayo
WETCU LTD inadaiwa na vyama vya msingi.
ü Je, Gari hilo aina ya ZX-V8
linatija gani katika kuboresha maisha ya mkulima wa Tumbaku ambaye anakabiliwa
na changamoto nyingi za kinyonyaji.
ü Ni kwa nini Bodi ya WETCU LTD isingesubiri
Mkutano Mkuu wa 23 ili wanachama watathmini umuhimu wa kununua Gari hilo.
ü Taarifa ya mwenyekiti wa Bodi ya
WETCU LTD imeeleza kuwa fedha zilizotumika kununulia gari zilitokana na faida
ya shilingi milioni 407,738,520/- baada ya kuuza
na kununua Hisa katika Soko la Hisa (DSE),Kama hali ni hiyo zile shilingi
milioni 40 zilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa Gari zilikwenda wapi na kwa
idhini ya nani?
ü Kwa nini fedha hizo zisingetumika
kulipa madai ya wafanyakazi wa WETCU LTD ambao walipeleka shauri lao Mahakama
Kuu kitengo cha kazi.
2) Taarifa ya mwenyekiti wa Bodi ya
WETCU LTD iliwataka wajumbe wa Mkutano huo waridhie kuchangia dola za Kimarekani
1.04 kwa kila bei ya mfuko wa mbolea ya NPK, CAN na UREA ili kumalizia deni
lililobaki la Shilingi milioni 556,150,524/-
Hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa Mkutano huo:-
ü Licha ya Bodi ya WETCU LTD kufanya
biashara ya kuuza na kununua Hisa na kupata faida ya shilingi milioni 407,738,520/- iliona ni muhimu kununua Gari na kufanya
mambo mengine badala ya kupunguza mzigo kwa mkulima wa Tumbaku kwa makato
yasiyokwisha.
3) Taarifa ya mwenyekiti wa Bodi ya
WETCU LTD imeeleza kuwa walifanikiwa kuuza hisa zao staili milioni 6 katika
Soko la HISA (DSE) na Kuingiza kiasi cha shilingi bilioni 2,507,738,520/- kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi
bilioni 2,100,000,000/- zilitumika kununua idadi
ya HISA stahili (Right Issue) milioni 6, na hivyo kupata faida ya shilingi
milioni 407,738,520/-
Mkutano
mkuu wa 22 wa mwaka 2015 ulipisha azimio la kuuza HISA milioni 6 kati ya
milioni 36 zilizowekezwa na WETCU LTD katika benki ya CRDB pamoja na mchango wa
dola za Kimarekani 1.04 kwa kila bei ya mfuko wa NPK, UREA na CAN.
Mauzo
ya HISA yaliingiza jumla ya Shilingi bilioni 2,491,909,000/-
na makusanyo ya dola ya Kimarekani kwa bei ya mfuko wa mbolea yaliingiza
Shilingi 718,447,680/-
Hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa Mkutano huo:-
ü Kama makusanyo ya dola za
Kimarekani 1.04 kwa kila bei ya mfuko wa mbolea ya NPK,UREA na CAN yaliingiza
shilingi milioni 718,447,680 kwa mwaka 2015,
wakati deni lililobaki ni milioni 556,150,524/-, Je
fedha itakayozidi kwenye makusanyo hayo kwa mwaka 2016 itakwenda wapi na kwa
idhini ya nani.
4) Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika
aliwaambia wajumbe wa Mkutano huo kuwa ofisi yake iliidhinisha ombi la WETCU
LTD la kutumia faida ya mauzo na manunuzi ya HISA milioni 6 kwa ajili ya
kununulia Gari aina ya ZX-V8.
Hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa Mkutano huo:-
ü Mamlaka ya kisheria aliyonayo Mrajisi
wa Vyama vya Ushirika yalitathmini mahitaji ya wanachama wa WETCU LTD ambavyo
ni vyama vya msingi vya Ushirika kabla ya kutoa uamuzi huo?
ü Je Mrajisi alijiridhisha kwa
kiwango gani kuwa ununuzi wa Gari hilo utakuwa na tija kwa wanachama wa WETCU
LTD.
ü Je, Mrajisi alikuwa na haraka
gani kuidhinisha fedha hizo zitumike kununua Gari badala ya kulipeleka suala
hilo kwenye mkutano mkuu ili lijadiliwe na wanachama.
ü Je, Mrajisi kwa kitendo cha
kuidhinisha Bodi ya WETCU LTD kununua Gari badala ya vipaumbele vingine ana lengo
la kuimarisha Ushirika?
No comments:
Post a Comment