WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,
WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
MAADHIMISHO YA SIKU YA
WANAWAKE DUNIANI:8 MACHI, 2016
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na watoto inawataarifu wananchi wote kuwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka
Tanzania huungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha
Siku ya Wanawake Duniani.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake, hutoa fursa
kwa Serikali, wananchi, wadau, na wanawake wenyewe kupima utekelezaji wa
maazimio, matamko na mikataba ya Kimataifa, Kikanda na Kitaifa inayohusu
masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa jinsia.
Siku
ya wanawake Duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani,
kuhamasisha jamii kutafakari kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake ya
kila mwaka; kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na
Serikali na asasi mbalimbali yakiwemo Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika
kuwaendeleza wanawake; na kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa sera na
mipango mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kudumisha Amani, Usawa na
Maendeleo.
Kaulimbiu
ya kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani mwaka 2016 inasema “50
– 50 Ifikapo 2030; Tuongeze Jitihada”. Kaulimbiu
hii inasisitiza kuwa na mikakati thabiti yenye mwelekeo wa kufikia Agenda 2030 ya malengo inayohimiza kufikia asilimia
50 kwa 50 ya ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja zote za maendeleo.
Kuanzia
mwaka 2005 Serikali ilipitisha uamuzi kuwa, maadhimisho haya yafanyike Kitaifa
kila baada ya miaka mitano kutoa muda wa utekelezaji wa maazimio na kupima
mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano. Mwaka 2015 Maadhimisho
yalifanyika Kitaifa mkoani wa Morogoro.
Kwa mwaka 2106, mikoa yote itaadhimisha siku hii katika maeneo yao kwa kuzingatia hali na mazingira ya mikoa husika.
Kwa mfano mkoa wa Dar es salaam, utaadhimisha siku hii katika Manispaa ya Kinondoni. Wizara inatoa wito kwa mikoa yote kuhamasisha wananchi na wadau wote kushiriki maadhimisho ya siku hii adhimu na kuzingatia ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka 2016.
Kwa mwaka 2106, mikoa yote itaadhimisha siku hii katika maeneo yao kwa kuzingatia hali na mazingira ya mikoa husika.
Kwa mfano mkoa wa Dar es salaam, utaadhimisha siku hii katika Manispaa ya Kinondoni. Wizara inatoa wito kwa mikoa yote kuhamasisha wananchi na wadau wote kushiriki maadhimisho ya siku hii adhimu na kuzingatia ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka 2016.
Rai
yangu kwa wadau wote ni kuwa, tuunge mkono jitihada za Serikali katika kutoa
haki na ushiriki sawa katika fursa za uongozi wa kisiasa na kiuchumi; na kupima
mafanikio yaliyofikiwa na kuweka mipango yenye matokeo makubwa, na kubainisha
shuhuda za wanawake waliotoa mchango uliotukuka katika kuwezesha maendeleo ya
wanawake wenywe na taifa kwa ujumla.
Nashauri wanahabari wote kuelimisha jamii kuhusu
kaulimbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2016 ili kila mwananchi aweze kutambua
jukumu alionalo katika kufikia lengo la ushiriki sawa wa wanawake na wasichana katika uchumi; afya, elimu, ajira,
sheria na siasa ifikapo mwaka 2030.
Nawatakia mafanikio mema katika maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu.
Sihaba Nkinga
KATIBU MKUU
3/3/2016
No comments:
Post a Comment