Azam FC ya Tanzania Jumamosi imeonyesha umwamba ugenini baada ya
kuwatungua wapinzani wao Bidvest Wits ya Afrika kusini kwa magoli 3 kwa bila
katika mechi ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho ikiwa mechi ya mkondo wa
kwanza.
Bidvest Wits waliingia uwanjani kuikabili Azam FC huku wakiwa na
rekodi ya ushindi mnono wa jumla ya mabao 9 kwa 0 dhidi ya timu ya Light Stars
ya Seychelles waliyoiondoa katika mzunguko wa kwanza.
Mechi hiyo iliwapeleka Azam FC na Bidvest Wits bila kufungana
katika kipindi cha kwanza, lakini kipindi cha pili kilitumiwa vyema na Azam FC
ambapo walizifumania nyavu za wapinzani wao mara tatu ndani ya dakika 9 tu.
Alikuwa ni Salum Abubakar ambaye alifungua ukurasa wa magoli
pale alipoachia shuti la mbali katika dakika ya 51 na kuandika goli la kwanza,
dakika tano baadae Shomari Kapombe aliifungia Azam FC bao la pili na
mshambuliaji John Bocco alifunga ukurasa wa magoli kwa kupachika bao la 3
katika dakika ya 59.
Bidvest Wits watakuwa wakiupanda mlima katika mechi ya pili ya
marudiano itakayopigwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ambapo watahitaji
kufunga mabao kuanzia 4 kwa bila ili waweze kusonga mbele.
Mbabe baada ya mechi ya marudiano kati ya Azam FC na Bidvest
Wits atakutana na mshindi wa mechi ya Esperance ya Tunisia na Renaissance ya
Madagascar.
Katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Jumamosi nchini
Madagascar timu ya Esperance ya Tunisia ilishinda ugenini kwa magoli 2 kwa 0
dhidi ya Renaissance.
Kwa matokeo ya mechi za mkondo wa kwanza kuna uwezekano mkubwa
wa Azam FC kukutana na timu
machachari ya Esperance ya
Tunisia.
MATOKEO YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA ( CAF CONFEDERATION CUP)
JUMAPILI 13 MACHI,
2016
|
1.
|
|
1-0
|
|
2.
|
|
2-1
|
El
Ahly Shandy
|
3.
|
|
1-0
|
|
JUMAMOSI 12 MACHI,2016
|
1.
|
|
3-0
|
|
Barrack Young Controllers
|
|
2.
|
|
0-2
|
|
3.
|
Bidvest
Wits
|
0-3
|
|
4.
|
Misr
Makkassa
|
3-1
|
|
5.
|
|
2-0
|
|
6.
|
|
0-0
|
|
7.
|
|
1-0
|
|
Liga Desportiva de Maputo
|
|
8.
|
|
0-2
|
|
9.
|
|
4-0
|
JKU
SC
|
10.
|
Atletico
Olympic
|
0-2
|
|
11.
|
|
1-2
|
|
12.
|
|
2-1
|
|
IJUMAA 11 MACHI,2016
|
1.
|
UMS
de Loum
|
1-1
|
|
No comments:
Post a Comment