Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Tuesday, March 29, 2016

MACHINJIO YA MJI WA TABORA YAFUNGWA KWA SIKU ZISIZOJULIKANA

Na,Thomas Murugwa  Tabora.
Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA  imeifunga machinjio  ya nyama ya mjini Tabora kwa muda usiojulikana baada ya kushindwa kutekeleza makubaliano ya kuondoa uchafu na kukarabati mifumo ya maji safi na maji taka ili kunusuru afya za walaji.

Kaimu meneja wa mamlaka hiyo kanda ya Magharibi Dr Edgar Mahudi amesema wamefikia hatua hiyo baada ya uongozi wa  halmashauri ya Manispaa ya Tabora pamoja na mambo mengine kushindwa kufanya usafi kama walivyoagiza siku saba zilizopita.


Amesema kuwa TFDA  iliipa manispaa hiyo wiki moja  iwe imekarabati mifumo ya maji safi na maji taka pamoja na kuondoa uchafu uliokuwa umerundikana katika maeneo ya machinjio hayo.

Dr. Mahundi  amebainisha kuwa uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora ulichokifanya ni kuweka bomba la maji na kupima afya za watumishi wa machinjio hiyo pasipo kufanya usafi wa eneo linalozunguka machijio hiyo.

Ameyataja baadhi ya mambo ambayo hayakutekelezwa ni pamoja na kuchimba shimo la maji taka, eneo la kutupia kinyesi cha ngombe  baada ya kuchinjwa , ukarabati wa jengo la banda la kuhifadhia ngozi pamoja na jengo linalotumika kuhifadhia mifugo kabla ya kuchinjwa.

Aidha Dr. Mahundi  amebainisha kuwa mamlaka hiyo iliagiza ujengwe uzio wa machinjio hiyo ambao umechakaa ikiwa ni pamoja na kuweka lango kuu moja ili kuzuia wizi wa mifugo.

Ameongeza  kuwa katika machinjio hiyo kunahitajika  vifaa kwa ajili ya
kupimia mifugo ili kuibaini kama ina magonjwa au haina na kwamba
utaratibu wa sasa wa upimaji umekuwa na kasoro kadhaa.

Afisa afya wa mkoa wa Tabora  Dr. Sanga Ulanzimila amesema kuwa hali ya usafi katika machinjio hiyo ni mbaya na walishatoa maelekezo kwa wahusika wake lakini wanashangaa kuona hawakuzingatia hadi TDFA wamelazimika kuifunga.




No comments: