Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, March 13, 2016

PELLEGRINI AWATAKA WACHEZAJI WA MANCHESTER CITY KUZINGATIA MECHI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA



Pellegrini
Kocha wa timu ya Manchester City Manuel Pellegrini amewataka wachezaji wake kuelekeza nguvu zao kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kupata matokeo tasa dhidi ya Norwich City kwenye ligi kuu ya Uingereza EPL iliyochezwa kwenye uwanja Carrow Road Jumamosi.

Kauli ya kocha huyo ni dhahiri ameanza kupoteza matumaini ya kuutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza kutokana na Manchester City kuachwa pointi 9  na vinara wa ligi hiyo Leicester City ambao wanacheza Jumatatu na Newcastle United inayoongozwa na Rafael Benitez.

Pellegrin amesema kipaumbele kwa timu yake ya  Manchester City ni mechi ya Jumanne wiki ijayo ambapo itakuwa Etihad kuivaa Dynamo Kiev katika mechi ya mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya huku ikiongoza kwa mabao 3 kwa 1 kwa matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza.

No comments: