Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Monday, March 14, 2016

EPL:LEICESTER CITY HAIKAMATIKI YAJIKITA KILELENI



 
SHINJI OKAZAKI

Leicester City imeendelea kuongeza pointi za kukaa kileleni mwa ligi kuu ya nchini Uingereza EPL baada kuifunga Newcastle United  goli 1 kwa 0 kwenye mechi iliyochezwa Jumatatu kwenye uwanja wa King Power.

Wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki wao Leicester City ilipata bao hilo la pekee kupitia kwa Shinji Okazaki katika dakika ya 25 ambaye alipiga tiktaka akiwa kwenye eneo la hatari kwenye lango la wapinzani wao.

Leicester City imefikisha pointi 63, pointi 5 zaidi ya zile za Tottenham Hotspur ambayo inapointi 58 ikiwa nafasi ya pili,pia imeiacha Arsenal kwa pointi 11 ikiwa na nafasi ya tatu na imetengeneza tofauti ya pointi 12 na Manchester City iliyoko nafasi ya nne.

Arsenal na Machester City kila timu inamchezo mmoja mkononi.

Kocha wa Newcastle United, Rafael Benitez ambaye amerithi mikoba ya Steve McClaren Ijumaa iliyopita ameangukia pua katika mechi yake ya kwanza akiwa na klabu hiyo ambapo pia atakuwa na kibarua kigumu Jumapili ijayo pale atakapokutana na Sunderland.

Newcastle United imecheza mechi 29 na imejikusanyia pointi 24 na iko nafasi ya 19 kati ya timu 20 za ligi hiyo.

No comments: