Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Wednesday, March 30, 2016

YANGA, AZAM FC UWANJANI ROBO FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO



Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inaendelea tena Alhamis ya Tarehe 31 Machi, 2016 ambapo Yanga wataikaribisha Ndanda FC kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku Azam FC wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini humo.

Robo fainali ya kwanza ilichezwa tarehe 26 Machi, 2016 ambapo Geita Gold walikuwa wenyeji wa Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.Mwadui FC ilikuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Geita Gold kwa magoli 3 kwa 0.

Mechi ya mwisho ya robo fainali itachezwa tarehe 6 April,2016 ambapo Simba itacheza dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Droo ya nusu fainali ya kombe hilo itachezeshwa na kupangwa tarehe 7 April,2016.

Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu, ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) 2017.

AFISA MTENDAJI WA KIJIJI APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA TSH 50,000/-




Na Thomas Murugwa, Tabora.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Tabora imemkamata na kumfikisha mahakamani afisa mtendaji wa kijiji Utimle wilayani Sikonge kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi elfu 50,000/-.

Akisoma mashitaka dhidi ya mshitakiwa huyo Batholomeo Athanas Sonda mbele ya hakimu wa mahakama ya mkoa wa Tabora Jackton Rushwela wakili wa TAKUKURU Edson Mapalala alisema mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo mjini Sikonge kati ya tarehe mosi na pili Machi mwaka huu.

Wakili huyo wa TAKUKURU  alidai mahakamani hapo kuwa mtendaji huyo wa kijiji mnamo tarehe 1 Machi 2016  akiwa kwenye eneo la stendi ya mabasi ya Sikonge aliomba shilingi laki nne kutoka kwa Hussein Hamis Swalehe ili amruhusu aendelee kuvuna mazao ya misitu.

 Ilidaiwa katika shitaka la pili kuwa mtuhumiwa alipokea shilingi elfu 50,000/= toka kwa Swalehe ikiwa kama kishawishi ili amruhusu aendelee kuvuna mazao ya misitu bila kuwa na kibali toka kwa mkurugenzi wa maliasili.

 Mtendaji huyo amekana makosa yote mawili  na kesi hiyo impangwa kutajwa tarehe 5 Aprili 2016 ili ipangiwe tarehe ya usikilizwaji wa awali.

Hakimu Rushwela alikubali mtuhumiwa apewe dhamana ya watu wawili kwa ahadi ya shilingi milioni tano na kutoa masharti kwamba mmoja wa wadhamini awe ni mkazi wa manispaa ya Tabora ili iwe rahisi kumpata mtuhumiwa pindi anapohitajika.

Masharti hayo yamewekwa na mahakama kwa kile kilichodaiwa  kuwa watuhumiwa wengi wanapodhaminiwa na wakazi  wa nje ya manispaa ya Tabora wamekuwa wanashindwa kufika mahakamani na hivyo inakuwa ni vigumu kuwapata ili wajibu mashitaka yao.

Hii ni mara ya pili kwa watendaji wa vijiji vya wilaya ya Sikonge kufikishwa mahakamani mkoani hapa wakikabiliwa na mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa katika kipindi kisichozidi wiki mbili.

Machi 23 mwaka huu  TAKUKURU iliwafikisha mahakamani Alfred Mashaka afisa mtendaji wa kata ya Kiloleli na Thomas Dickson afisa mtendaji wa kijiji cha Kanyamsenga kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi laki saba.

Tuesday, March 29, 2016

MACHINJIO YA MJI WA TABORA YAFUNGWA KWA SIKU ZISIZOJULIKANA

Na,Thomas Murugwa  Tabora.
Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA  imeifunga machinjio  ya nyama ya mjini Tabora kwa muda usiojulikana baada ya kushindwa kutekeleza makubaliano ya kuondoa uchafu na kukarabati mifumo ya maji safi na maji taka ili kunusuru afya za walaji.

Kaimu meneja wa mamlaka hiyo kanda ya Magharibi Dr Edgar Mahudi amesema wamefikia hatua hiyo baada ya uongozi wa  halmashauri ya Manispaa ya Tabora pamoja na mambo mengine kushindwa kufanya usafi kama walivyoagiza siku saba zilizopita.


Amesema kuwa TFDA  iliipa manispaa hiyo wiki moja  iwe imekarabati mifumo ya maji safi na maji taka pamoja na kuondoa uchafu uliokuwa umerundikana katika maeneo ya machinjio hayo.

Dr. Mahundi  amebainisha kuwa uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora ulichokifanya ni kuweka bomba la maji na kupima afya za watumishi wa machinjio hiyo pasipo kufanya usafi wa eneo linalozunguka machijio hiyo.

Ameyataja baadhi ya mambo ambayo hayakutekelezwa ni pamoja na kuchimba shimo la maji taka, eneo la kutupia kinyesi cha ngombe  baada ya kuchinjwa , ukarabati wa jengo la banda la kuhifadhia ngozi pamoja na jengo linalotumika kuhifadhia mifugo kabla ya kuchinjwa.

Aidha Dr. Mahundi  amebainisha kuwa mamlaka hiyo iliagiza ujengwe uzio wa machinjio hiyo ambao umechakaa ikiwa ni pamoja na kuweka lango kuu moja ili kuzuia wizi wa mifugo.

Ameongeza  kuwa katika machinjio hiyo kunahitajika  vifaa kwa ajili ya
kupimia mifugo ili kuibaini kama ina magonjwa au haina na kwamba
utaratibu wa sasa wa upimaji umekuwa na kasoro kadhaa.

Afisa afya wa mkoa wa Tabora  Dr. Sanga Ulanzimila amesema kuwa hali ya usafi katika machinjio hiyo ni mbaya na walishatoa maelekezo kwa wahusika wake lakini wanashangaa kuona hawakuzingatia hadi TDFA wamelazimika kuifunga.




MSIMAMO WA MAKUNDI YA KUFUZU FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA, AFCON 2017



Group A


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Liberia
4
3
0
1
8
2
6
9
2
Tunisia
4
2
1
1
9
2
7
7
3
Togo
4
2
1
1
4
2
2
7
4
Djibouti
4
0
0
4
1
16
-15
0
Group B


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Congo DR
4
3
0
1
6
4
2
9
2
Central African Republic
4
2
1
1
5
6
-1
7
3
Angola
4
1
1
2
5
4
1
4
4
Madagascar
4
0
2
2
3
5
-2
2
Group C


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Mali
4
3
1
0
5
1
4
10
2
Benin
4
2
2
0
8
4
4
8
3
South Sudan
4
1
0
3
3
8
-5
3
4
Equatorial Guinea
4
0
1
3
1
4
-3
1
Group D


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Burkina Faso
4
2
1
1
3
1
2
7
2
Uganda
4
2
1
1
3
1
2
7
3
Botswana
4
2
0
2
3
4
-1
6
4
Comoros
4
1
0
3
2
5
-3
3
Group E


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Guinea-Bissau
4
2
1
1
4
4
0
7
2
Congo
4
1
3
0
7
5
2
6
3
Zambia
4
1
3
0
4
3
1
6
4
Kenya
4
0
1
3
2
5
-3
1
Group F


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Morocco
4
4
0
0
7
0
7
12
2
Cape Verde
4
2
0
2
9
5
4
6
3
Libya
4
1
0
3
6
5
1
3
4
Sao Tome
4
1
0
3
3
15
-12
3
Group G


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Egypt
3
2
1
0
5
1
4
7
2
Nigeria
3
0
2
1
1
2
-1
2
3
Tanzania
2
0
1
1
0
3
-3
1
Group H


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Ghana
4
3
1
0
11
2
9
10
2
Rwanda
4
2
0
2
6
2
4
6
3
Mauritius
4
2
0
2
3
12
-9
6
4
Mozambique
4
0
1
3
1
5
-4
1
Group I


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Gabon
4
2
1
1
6
2
4
7
2
Ivory Coast
4
1
3
0
2
1
1
6
3
Sierra Leone
4
1
1
2
2
3
-1
4
4
Sudan
4
1
1
2
2
6
-4
4
Group J


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Algeria
4
3
1
0
17
5
12
10
2
Ethiopia
4
1
2
1
7
12
-5
5
3
Seychelles
4
1
1
2
4
7
-3
4
4
Lesotho
4
1
0
3
4
8
-4
3
Group K


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Senegal
4
4
0
0
9
2
7
12
2
Burundi
4
2
0
2
7
7
0
6
3
Namibia
4
1
0
3
4
7
-3
3
4
Niger
4
1
0
3
2
6
-4
3
Group L


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Zimbabwe
4
2
2
0
8
3
5
8
2
Guinea
4
1
2
1
4
4
0
5
3
Swaziland
4
1
2
1
5
8
-3
5
4
Malawi
4
0
2
2
4
6
-2
2
Group M


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Cameroon
4
2
2
0
4
2
2
8
2
Mauritania
4
2
1
1
5
3
2
7
3
South Africa
4
0
3
1
3
5
-2
3
4
Gambia
4
0
2
2
1
3
-2
2