Na
Lucas Raphael,Nzega
Kata ya Bukene wilaya ya Nzega mkoani Tabora
imekusudia kumaliza tatizo la madawati katika shule za msingi na sekandari
katika katani humo kwa kuchonga madawati 500 nyenye thamani ya shilingi
milioni 50.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mtendaji
wa kata hiyo Daniel Kapama amesema kwamba kusudio hilo lilifikiwa kwenye kamati
ya maendeleo ya kata kwa kuwashirikisha na wananchi wenyewe.
Amesema kwa kila mjumbe wa kamati hiyo hatachangia
dawati moja na diwani wa kata hiyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya
maendeleo hatachingia madawati mawili.
Kapama amebainisha kuwa kamati hiyo ilipendekeza kumuona afisa maliasilia
ili kutoa kibali cha kuchana mbao kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo la
madawati kabla ya Juni 30 mwaka huu.
Amesema kwamba madawati hayo yatasaidia kuondoa
tatizo la kukaa chini ambalo limeongezeka baada ya kuandikishwa watoto 680 kuanza
darasa la kwanza na wale wa awali ni watoto 425.
Kapama amesema kutokana na idadi hiyo ya
wanafunzi imepelekea kuongezeka kiwepo kwa upungufu wa madawati kwa baadhi ya
shule katika kata hiyo.
Aidha Diwani wa kata hiyo Omary shabani Omary amesema
katika maazimio yao pia wamedhamiria kujenga madarasa 4 ya shule ya msingi
Bukene na jengo la utawala shule ya sekondari Bukene.
Amesema kwamba pia wamepanga kukamilisha ujenzi wa
nyumba ya sekondari Bukene ambapo kila mjumbe wa kamati ya maendeleo ya kata
atachangia mfuko moja wa saruji na wananchi watangia kiasi cha
shilingi 4,100/=.
Omary ameeleza kwamba yeye diwani atachangia
mifuko miwili ya saruji na wafanyabiashara wataungana wawili wawili kwa
ajili ya kuchangia mfuko moja wa saruji .
No comments:
Post a Comment