NA Thomas Murugwa,Tabora.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Emanuel Ngigwana amesema mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha pasipo shaka maombi yake yote matano ili mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi mgombea huyo wa CHADEMA.
Amesema kuwa mlalamikaji alishindwa kuleta ushahidi wa kuunga mkono madai yake ikiwemo kujaza fomu za malalamiko ya kupinga matokeo ya vituo husika hata kupitia kwa mawakala wake.
Hakimu huyo ameeleza kuwa katika kesi za uchaguzi,mlalamikaji amepewa jukumu la kuthibitisha pasipo shaka yoyote madai yake dhidi ya mlalamikiwa jambo ambalo mlalamikaji katika shauri hilo ameshindwa kufanya hivyo.
Pamoja na kutupilia mbali madai hayo mahakama ilimthibitisha Machibya
wa CHADEMA kuwa diwani halali wa kata hiyo na imemtaka mlalamikaji huyo Julius Salawe alipe gharama za uendeshaji wa shauri hilo.
Mahakama hiyo pia imetubilia mbali madai ya Suleiman Denis Onesmo wa CHADEMA aliyetaka kutenguliwa kwa ushindi wa diwani wa kata ya
Silambo,Wilayani Kaliua Ibrahim Issaya Kifoka wa CCM na kumthibitisha yeye kuwa diwani halali.
Hakimu Ngigwana katika uamuzi wake uliochukua saa mbili amesema
Mlalamikaji ameshindwa kuithibitishia mahakama pasipo shaka madai yake kwa kuleta ushahidi hafifu ulioshindwa kutengua ushindi wa Kifoka.
Akisoma uamuzi huo hakimu Ngigwana amesema madai kuwa mlalamikiwa wa kwanza Kifoka alipeleka kura bandia 68 katika moja ya kituo cha kupigia kura hayakuthibitishwa na mlalamikaji kwani kura hizo bandia hazikuwasilishwa mahakamani hapo kama kielelezo.
Hakimu huyo amesema kwa ufupi mlalamikaji hakuwa na ushahidi
wenye nguvu huku ushahidi wake ukiwa ni wa kusikia na kuelezwa na watu akiwemo wakala wake.
katika madai Kwamba mlalamikiwa alimtumia mtoto wake Issaya Kifoka
kumsimamia, mahakama ameona kuwa hilo halijathibitishwa na upande wa mlalamikaji kama ni kosa kwani hata mdai alimtumia ndugu yake Paul Dennis kuwa wakala.
Kutokana na kitendo cha mlalamikaji kushindwa kuthibisha madai yake
mahakama ilimthibitisha Ibrahim Kifoka kuwa diwani halali wa kata ya
Silambo na kuwataka wahusika kuendelea kuishi kwa amani kwani baada ya uchaguzi maisha lazima yaendelee.
No comments:
Post a Comment