Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, April 3, 2016

COASTAL UNION YAZIDI KUTOTA, YANGA YABEBWA KWA VISINGIZIO


MATOKEO YA VPL

JUMAMOSI 2 APRIL,2016
1.
Mbeya City
4-0
Coastal Union
2.
Mwadui
1-2
Mtibwa Sugar
JUMAPILI 3 APRIL,2016
1.
Young African
V
Kagera Sugar
2.
V
3.
V
4.
V
5.
v

YANGA YABEBWA KWA VISINGIZIO

Siasa za Soka la Bongo kila kukicha zinachukua sura mpya baada ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF kukubali kuisogeza mbele mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar iliyopangwa kuchezwe Jumatano tarehe 6 April,2016 na badala yake itachezwa tarehe 16 April,2016 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya klabu ya Yanga kulalamika kupangiwa mechi tatu ndani ya wiki moja kabla ya kuvaana na Al Ahly ya Misri Jumamosi ijayo ya terehe 9 April,2016 kwenye kinyang’anyiro cha ligi ya Mabingwa Afrika.

Swali la kujiuliza Madai hayo ya Klabu ya Yanga yanamsingi wowote katika soka la kisasa linalotawaliwa na uwekezaji wa rasilimali fedha,vifaa,watu na maarifa.

Kama kweli tunataka kuimarisha Soka la Bongo inatupasa kuacha visingizio, hoja na mitazamo ya kisiasa mahali tunapotakiwa kuonyesha vitendo na uwezo zaidi.

Chukua mfano huu Jumamosi April 2,2016 Barcelona na Real Madrid zimecheza mechi yao ya ligi inayojulikana kama “El Clasico” ambapo Real Madrid iliishinda Barcelona kwa magoli 2 kwa 1.

Kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Jumanne April 5,2016 Barcelona itakuwa kwenye uwanja wa nyumbani Camp Nou kuikaribisha Atletico Madrid ikiwa ni hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Aidha Jumatano April 6,2016 Real Madrid itakuwa ugenini kwenye uwanja wa “Volkswagen Arena” kuivaa VfL Wolfsburg kwenye UEFA Champions League.

Timu hizo vigogo kwenye ligi kuu ya Hispania zitashuka Dimbani kwa mara nyingine Jumamosi ya tarehe 9 April,2016 ambapo Barcelona itasafiri hadi kwenye uwanja wa Anoeta kucheza na Real Sociedad, wakati Real Madrid itakuwa nyumbani Santiago Bernabeu wakiikaribisha timu ya Eibar.

Hii inamaana kuwa timu hizo za Barcelona na Real Madrid zinashuka dimbani mara tatu ndani ya wiki moja na  hatujasikia zikilalamikia ratiba au kupewa muda wa kujiandaa na UEFA Champions League.

Utaratibu huo makini uliowekwa na watu wenye mikakati na mtazamo wenye kuzingatia weledi wa taaluma, biashara na uwekezaji wa hali ya juu unaonekana dhahiri kwenye ligi za Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Italia na nchi nyingine zilizopiga hatua kisoka.

Kama utaratibu huo unawezekana mahali pengine duniani na timu zinafanya vizuri ni kipi kinashindikana kwa Yanga ambayo inanolewa na  kocha wa kigeni muholanzi Hans van der Pluijm.

Yanga pia imesheheni wachezaji wa kimataifa akiwemo Vincent Bossou (Togo) , Donald Ngoma, Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima (Rwanda), Andrey Coutinho (Brazil) na Amis Tambwe (Burundi).

Kwangu mimi naona tunayosafari ndefu ya kufikia mafanikio ya KWELI katika mchezo wa soka wenye mashabiki wengi, fedha nyingi na uwekezaji mkubwa kama timu zetu zitaendelea na siasa za kubebwa na kuonewa huruma.

No comments: