Meneja wa timu ya Al Ahly “Red
devils” ya nchini Misri Martin Jol ametangaza kikosi cha wachezaji 11 kitakachoivaa
Yanga ya Tanzania katika mechi ya marudiano ya ligi ya Mabingwa barani Afrika itakayochezwa
majira ya saa 19:30 kwa saa za Misri.
Mechi hiyo ya hatua ya 16 bora
itachezwa leo Jumatano kwenye uwanja wa Borg El-Arab katika mji wa Alexandria.
Meneja huyo Martin Jol ametangaza
kikosi hicho kuwa na wachezaji ambao ni Sherif Ekramy;Ahmed Fathi,Rami
Rabia,Ahmed Hegazy,Sabry Rahil;Hossam Ashour;Hossam Ghaly;Abdallah
El-Said,Momen Zakaria,Ramadan Sobhy na Amr Gamal.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa
jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya bao 1 kwa 1.
Martin Jol ni mholanzi mwenye umri
wa miaka 60 ni kocha wa zamani wa ligi kuu ya Uingereza ambapo amewahi kuzinoa
timu za Tottenham
Hotspur na Fulham.
Kocha huyo pia amewahi kuifundisha
klabu ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi na Humburger SV ya Ujerumani.
Hans van der Pluijm ni kocha wa
klabu ya Yanga ya Tanzania amezaliwa tarehe 3 Januari, 1943 katika eneo la Nieuwkuijk,
nchini Uholanzi.
Amewahi
kuzifundisha timu kadhaa ikiwemo FC Den Bosch na amekuwa nchini Ghana tangu
mwaka 1999.
Kabla ya
kujiunga na Yanga amewahi kuzifundisha timu za Medeama SC, Berekum Chelsea
ambapo kwa timu za Heart of Lions na Ashanti Gold
amezinoa kwa misimu tofauti.
No comments:
Post a Comment