Na,
Thomas Murugwa, Tabora.
Elisha Seif David aliyekuwa askari wa jeshi la polisi kituo kidogo cha polisi King’wangoko tarafa ya Ulyankulu wilaya ya Kaliua mkoani Tabora hajulikani haliko baada ya kupata taarifa ya kukamatwa na kushitakiwa kwa tuhuma ya Rushwa.
Elisha
ni miongoni mwa askari polisi wanne ambao wanadaiwa kumbambikia mche wa bhangi Dotto Gandulenya mkazi
wa kijiji cha Ilege tarafa ya Ulyankulu wilayani humo na kisha kulazimisha wapewe
shilingi milioni tatu ili wamuachie huru.
Askari
polisi wengine watatu waliohusika kwenye tukio hilo ambalo lililopelekea Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
-TAKUKURU kuingilia kati ni John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robert.
Taarifa
kutoka ndani ya jeshi la polisi wilaya
ya Kaliua zimeeleza kuwa askari huyo alikimbia kituo chake cha kazi baada
ya kutakiwa kufika ofisi ya mkuu wa polisi wilayani humo – OCD kati kati ya
mwezi uliopita.
Askari
hao waliofukuzwa kazi tayari wamekabidhiwa
mikononi mwa TAKUKURU ambayo imewafikisha mahakamani wakikabiliwa na
tuhuma mbili za kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu namba 15 (1) na (2)
cha sheria namba 11/2007 ya TAKUKURU.
Licha
ya hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Urambo Hamis Momba kuweka
masharti magumu ya dhamana Katika shauri hilo la jinai namba 78/2016 waliweza
kutimiza na wapo nje hadi aprili 27 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment