Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Monday, March 28, 2016

MCHUNGAJI LUTENGANO: "WATANZANIA TUMUUNGE MKONO RAIS MAGUFULI"

Na Allan Ntana, Tabora.

WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono jitihada zote zinazofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwa ameonyesha dhamira ya dhati ya kuiletea maendeleo makubwa nchi yetu.

Wito huo umetolewa na mchungaji Lutengano Asajile Mwasongela wa kanisa la TAG- Maranatha lililopo mtaa wa Cheyo B katika manispaa ya Tabora wakati wa mahojiano maalum katika kongamano la wanafunzi waliookoka lililofanyika Jumamosi katika ukumbi wa shule ya sekondari New Era.

Amesema heshima ya nchi imeanza kurudi, mwelekeo wa kiuchumi umeanza kuonekana, wabadhirifu wa mali za umma na wote wanaotumia madaraka vibaya wameanza kushughulikiwa ipasavyo ikiwemo kutumbuliwa majipu hali inayorejesha nidhamu ya kazi.

Mchunguji huyo amesema, “Sasa naionaTanzania mpya, makusanyo ya kodi yameanza kuonekana kwa kasi, kila taasisi ya serikali sasa inawajibika ipasavyo, uwajibikaji na nidhamu ya watumishi wa umma kwa wananchi imeanza kurudi, kwa kweli Rais anastahili pongezi.”

Amebainisha kuwa kasi ya utendaji wa Rais Magufuli inasifika ndani na
nje ya nchi na hata katika mitandao ya kijamii ya kitaifa na kimataifa
utakuta mijadala mingi inayogusa moja kwa moja kazi nzuri inayofanywa
na rais wetu.

Mchungaji Lutengano amefafanua, “Naomba sana Watanzania wote tumuunge mkono kwani ameifanya nchi yetu kuwa mfano wa kuigwa na viongozi wa mataifa mengine hapa duniani, lakini pia amedhihirisha wazi kuwa yeye ni Rais wa watu wote na hajali itikadi za vyama.”

Aidha amepongeza hatua iliyochukuliwa na Waziri wa Elimu Prof. Joyce
Ndalichako ya kurudisha mfumo wa zamani wa divisheni mashuleni kwani
unarahishaji hata upangaji madaraja kwa wanafunzi.

Mchungaji Lutengano amemuomba Rais Magufuli kupitia Waziri huyo kuzikarabati shule zote kongwe hapa nchini ili zirudi katika kiwango chake cha zamani kwa kuwa zimechakaa sana. 

Amezitaja baadhi ya shule hizo kuwa ni Tabora Girls’,Tabora Boys, Kazima, Milambo, Loleza, Ilboru, Moshi Tech, Ifunda na nyinginezo.

TFF YAAGIZA CHAMA CHA SOKA MKOA WA KATAVI KUCHUNGUZA USHINDI WA MAGOLI 16 KWA 0



RAIS WA TFF JAMALI MALINZI
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeagiza Chama Cha Soka Mkoa wa Katavi (KRFA) kufanya uchunguzi wa matokeo ya timu ya Stand FC kuibuka na ushindi wa magoli 16 kwa 0 dhidi ya Kamazima wakati wa mechi ya kuamua bingwa wa mkoa wa Katavi.

Mechi hiyo ilichezwa Jumamosi ilikuwa ya kuhitimisha kumpata bingwa wa mkoa huo atakayewakilisha kwenye ligi ya mabingwa mkoa ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kabla ya mchezo huo uliotoa matokeo ya kushangaza, timu ya Nyundo FC ilikuwa inaongoza kwa kuwa na pointi 21 na magoli 24 ya kufunga ambapo Stand FC ilikuwa ikihitaji kufunga magoli 13 kwa 0 ili iweze kuwa mabingwa wa mkoa huo

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa kutokana na Stand FC kushinda kwa mabao 16, inaonyesha kuna dalili za kupanga matokeo, hivyo KRFA haitaruhusiwa kutangaza bingwa wa mkoa wa Katavi hadi uchunguzi utakapokamilika na TFF kujiridhisha na uchunguzi huo.

Hivi karibuni TFF ilizuia kuitangaza timu iliyopanda daraja kutoka Kundi C la Ligi Daraja la Kwanza kutokana na madai ya kuwepo kwa vitendo kama hivyo ambapo katika mechi za mwisho, Geita Gold Sport iliifunga JKT Kanembwa magoli 8-0, huku Polisi Tabora ikiifunga JKT Oljoro mabao 7-0.

Sunday, March 27, 2016

MECHI YA TAIFA STARS NA CHAD YAOTA MBAWA




Timu ya Chad iliyokuwa icheze na timu ya taifa ya Tanzania “Taifa “Stars” kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumatatu Jioni,haitofika Tanzania baada ya kujitoa katika kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2017 zitakazochezwa nchini Gabon.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa Jumapili na katibu mkuu wa chama cha Soka nchini humo FTFA Moctar Mahamoud kwenda Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF imeeleza kuwa Chad imeshindwa kufika Dar es Salaam kucheza mechi ya marudiano  kwa madai kuwa haina fedha za kuwawezesha kuendelea na mechi za kundi G.

Taifa hilo la Chad limejitoa baada ya kucheza mechi tatu za mzunguko wa kwanza, huku ikifungwa na timu zote, ambapo ikicheza ugenini ilifungwa na Nigeria bao 2 kwa 1,ikiwa kwenye ardhi ya nyumbani ikafungwa magoli 5 kwa 1 na Misri, na tarehe 23 mwezi huu ikashindwa kutamba mbele ya Tanzania baada ya kukubali kichapo cha bao 1 kwa bila ikiwa nyumbani.

Kwa hatua hiyo ya Chad,kundi G limebaki na timu tatu za Tanzania, Misri na Nigeria.

Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF kujitoa kwa Chad kumesababisha kufutwa kwa matokeo yote ya timu hiyo, na hivyo kulifanya kundi G kuongozwa na Misri ikiwa na pointi 4 badala ya 7, Nigeria ya pili ikiwa na pointi 2 badala ya 5 na Tanzania inashika mkia ikiwa na pointi moja badala ya  4.

Aidha CAF imeitoza Chad faini ya dola za kimarekani 20,000 pamoja na kupigwa marufuku kushiriki hatua za kufuzu fainali za AFCON  mwaka 2019.

Hata hivyo Misri ikiwa nyumbani katika mji wa Alexandria wataikaribisha Nigeria katika mechi ya marudiano itakayochezwa Jumanne ya tarehe 29 mwezi huu baada ya mechi ya kwanza kuchezwa katika mji wa Kaduna na kutoka sare ya kufungana bao 1 kwa 1.


Kujitoa kwa Chad kumeyabakiza mataifa 50 ya Afrika yakiwania nafasi 15 za kufuzu fainali hizo za AFCON  ambapo zitaungana na mwenyeji Gabon na kukamilisha idadi ya timu 16.

Timu zitakazoongoza katika makundi yote 13 zitafuzu moja kwa moja kwenye fainali hizo na washindi wa pili wawili bora kutoka miongoni mwa makundi 12 ukiondoa kundi la kwanza lenye timu mwenyeji Gabon zitafuzu pia.


Hata hivyo Kamati ya Utendaji ya Shirikisho La Soka Barani Afrika CAF Mnamo tarehe 15 Januari,2015 ilipitisha uamuzi kwamba timu zikibaki tatu kwenye kundi ni timu moja tu ambayo itaoongoza kundi hilo ndio itafuzu fainali za AFCON.

Timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” itashuka kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi ya tarehe 4 Juni, 2016 kucheza na Misri.

WAKAZI WA KATA YA MWINYI MANISPAA YA TABORA WALALAMIKIA KUONDOLEWA KILOMETA NANE ZA MATENGENEZO YA BARABARA



Na Paul Christian, Tabora.

Wakazi wa kata ya Mwinyi katika Manispaa ya Tabora wamelilalamikia baraza la madiwani wa halmashauri ya Manispaa hiyo kwa hatua yake ya kupunguza kilometa nane kati ya kilometa kumi za barabara zilizotengewa bajeti ya matengenezo katika maeneo korofi katani humo.

Mmoja wa wakazi wa kata hiyo Martha Mwijalubi amesema kitendo hicho kimefanywa kwa makusudi ili kuwakomoa wakazi wa kata hiyo kwa kumchagua diwani kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika uchaguzi mkuu uliopita.

“Wingi wa madiwani wa chama tawala wameamua kuondoa kilometa hizo za barabara na kuzigawa katika kata nyingine ambapo barabara zao hazijaathiriwa sana na mvua zinazoendelea kunyesha.”Amebainisha mkazi huyo.

Alipohojiwa kuhusu suala hilo diwani wa kata hiyo Martin Mussa Daniel kwa tiketi ya CHADEMA amekiri kuwa  kikao cha baraza la madiwani kilichoketi tarehe 23 na 24 Februari mwaka huu kwa kutumia wingi wa madiwani wa Chama Cha Mapinduzi kilipitisha maazimio ya kuondoa kilometa nane za matengezo ya barabara katika kata hiyo na kubakisha kilometa mbili tu.

“Kama mwakilishi wa kata hiyo nilijitahidi kujenga hoja ya kutetea kilometa zote kumi zibaki kama ilivyopendekezwa kwa kuwa eneo la Mwinyi lina wakazi wengi na barabara zake zimekuwa zikiathiriwa mara kwa mara wakati wa msimu wa mvua.”Amesema diwani huyo.

Martin amebainisha kuwa ni dhahiri madiwani wa CCM walikuwa wamejipanga kufanya hivyo kwa lengo la kudhoofisha uwakilishi wa wananchi unaotokana na kumchagua mtu wa chama cha upinzani.

Ameongeza,“Hali hii itaathiri sana maendeleo ya Manispaa ya Tabora kwa kutumia itikadi za kisiasa na wingi wa madiwani wa CCM kupitisha maamuzi ya kukomoa wananchi wenye vyama na wasio na vyama kwa maslahi duni ya kisiasa yanayolenga uchaguzi wa mwaka 2020.”

Saturday, March 26, 2016

AFCON 2017 HATUA YA MAKUNDI RWANDA,BURUNDI,MISRI ZAIBUKA KIDEDEA, TANZANIA NJIA PANDA



JUMAPILI 27 MACHI, 2016
1.
Mozambique
0-0
Ghana
FT
2.
Kenya
0-1
Guinea-Bissau
FT
3.
Botswana
2-1

Comoros
FT
4.
Benin
4-1
South Sudan
FT
5.
Congo
1-1

Zambia
FT
JUMATATU 28 MACHI,2016
1.
Tanzania
-
Chad
FT
2.

Zimbabwe
4-0
Swaziland
FT
3.
Central African Republic
2-1
Madagascar
FT
4.
Libya
4-0
Sao Tome
FT
5.
Equatorial Guinea
0-1
Mali
FT
6.
Sierra Leone
1-0
Gabon
FT
JUMANNE 29 MACHI,2016
1.
Malawi
1-2
Guinea
FT
2.
Lesotho
2-1
Seychelles
FT
3.
Rwanda
5-0
Mauritius
FT
4.
Ethiopia
3-3
Algeria
FT
5.

Niger
1-2
Senegal
FT
6.
Sudan
1-1
Ivory Coast
FT
7.
Namibia
1-3
Burundi
FT
8.

Liberia
5-0
Djibouti
FT
9.
Uganda
0-0
Burkina Faso
FT
10.
Gambia
0-0
Mauritania
FT
11.

Angola
0-2
Congo DR
FT
12.
Togo
0-0

Tunisia
FT
13.
Egypt
1-0
Nigeria
FT
14.
South Africa
0-0
Cameroon
FT
15.
Morocco
2-0
Cape Verde
FT