Na Paul Christian,Tabora.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Injinia Dkt. Charles Tizeba amefanya ziara ya
kikazi mkoani Tabora kwa lengo la kubaini changamoto zinazolikabili zao la
tumbaku.
Katika ziara hiyo waziri huyo ametembelea masoko ya zao yaliyofanyika kwenye
vyama vya msingi vya ushirika wa wakulima wa tumbaku vya Tumbi katika manispaa
ya Tabora na Ngulu wilayani Sikonge.
Akiwa kwenye masoko hayo ameweza kuzungumza na
wakulima,wateuzi (classifiers) , wanunuzi (blenders),viongozi wa vyama vya
ushirika, wajumbe wa bodi ya tumbaku Tanzania (TTB).
Akifanya majumuhisho ya ziara hiyo mbele ya wadau
wa zao hilo kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt Tizeba
ameagiza yafuatayo:-
·
-Makampuni yanayonunua tumbaku mkoani Tabora kuwalipa wakulima malipo
yao ya pili bila masharti yoyote.
·
-Bodi ya Tumbaku kufanya hesabu ya kilo
zilizokuwa zikikatwa na makampuni yanayonunua zao hilo kwa kile kinachodaiwa “mnyauko”
ambao unaosababisha uzito wa tumbaku kupungua kwa kuwa mnunuzi amechelewa
kuondoa Tumbaku yake kwenye Magodauni baada ya kuinunua, baada ya hesabu hiyo
makampuni yatawalipa wakulima kwa msimu huu na misimu mingine iliyopita.
· -
Mabenki yote yaandike mikataba yote
kwa lugha ya Kiswahili ili wakulima waweze kuielewa mikataba hiyo.
·
-Mabenki kuacha kuwaibiwa wakulima kwa
kucheza na ubadilishaji fedha kutoka dola ya kimarekani kwenda kwenye shilingi
ya Tanzania.
·
-Bodi ya Tumbaku Tanzania TTB kuhamisha
makao yake makuu kutoka Morogoro hadi mjini Tabora.
·
-Bodi ya Tumbaku Tanzania TTB kuacha
kuburuzwa na makampuni yanayonunua Tumbaku au Tobacco Council na badala yake
wasimamie sheria kikamilifu.
·
-Bodi ya Tumbaku Tanzania TTB kuanzia
msimu ujao wa masoko ifute kabisa matumizi ya mizani ya rula na aina zake zote
na badala yake itumike mizani ya electronic ili kuandoa wizi kupitia mizani.
·
-Bodi ya Tumbaku Tanzania TTB ipunguze
madaraja ya Tumbaku kutoka 72 ya sasa.
·
-Mabenki kuacha kuyaingiza makampuni ya
ununuzi wa Tumbaku kwenye mikataba ya mikopo kwenye vyama vya msingi.
·
-Mrajis wa vyama vya Ushirika nchini kuhakikisha
vyama vya msingi ahakikishe vyama vya Ushirika 105 kati ya 217 vilivyoko
hatarini kufutwa mkoani Tabora vinarejea kutoa huduma kwa wanachama wao badala
ya kuvifuta.
·
-Mrajis atapoteza ajira yake ikibainika
chama cha Ushirika au SACCOS imekufa.
· -
Kuanzia msimu ujao Chama Kikuu Cha
Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi WETCU LTD hakita endeshwa na fedha ya
makato ya moja kwa moja kutoka kwenye kila kilo ya tumbaku na badala yake
wataomba fedha kutoka vyama vya msingi ambavyo ni mwanachama wa WETCU LTD na
sio mkulima mmoja mmoja.
· -
Halmashauri ya Tumbaku (Tobacco
Council) sio chombo cha kisheria hivyo kisitumike kumkandamiza mkulima.
·
-Mkulima hatokatwa kilo moja (mara
mbili) kwa ajili ya uzito wa gunia analofungia tumbaku.
·
-Ni mara ya kwanza na ya mwisho kwa
mtendaji mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania kushindwa kufika kwenye ziara ya
waziri mwenye dhamana.
· -
Independent Famers (IF) na Association
ni marufuku kwa kuwa zilitumika kuua ushirika.
·
-Wakulima waache kuchanganya grade
tofauti za tumbaku kwenye mtumba mmoja.
·
-Wakulima wadhibitiwe kutorosha
tumbaku.
·
-Kwenye vyama vya Msingi akopeshwe
mkulima mmoja mmoja na sio kwa vikundi ili kila mmoja abebe mzigo wa kulipa
deni lake.
Waziri Tizeba amebaini yafuatayo katika ziara hiyo:-
ü -Uchaguzi wa
viongozi kwenye vyama vya Ushirika ni Vita kuliko hata kugombea Ubunge.
ü -Tumbaku
haijabadilisha maisha ya watu.
ü -Asilimia 90 ya
matatizo yaliyoko kwenye vyama vya msingi vya ushirika yamesababishwa na watu
walioko nje ya vyama hivyo na asilimia 10 ni wanachama wa vyama hivyo.
ü -Kwenye masoko wanunuzi
(Blenders) wanasauti kuliko wateuzi wa serikali (classifiers).
ü -Maofisa ushirika ni
chanzo cha kufa kwa vyama vya Ushirika.
ü -Mrajis ni chanzo
cha kufa kwa vyama vya ushirika kwa kuwa anaidhinisha mikopo,utoaji
fedha,bajeti na nk.
ü -Mabenki ni chanzo
cha kufa kwa vyama vya ushirika yanatumia uelewa mdogo wa wakulima kujinufaisha
kwa wizi.
ü -Bodi ya Tumbaku
Tanzania TTB ni chanzo cha kuua ushirika kwa kuwa imeshindwa kutimiza wajibu
wake.
ü -Tobacco Council
inaamua kila kitu na sio Bodi ya Tumbaku Tanzania.
ü Viongozi wa vyama
vya msingi wanaingia mikataba wasiyoijua au kuielewa.
ü- Mikopo ya mabenki
imekatiwa bima lakini vyama vya msingi vikishindwa kulipa mikopo hiyo bado
wanaendelea kudaiwa.
ü -Zabuni za
usambazaji Pembejeo zinatolewa kwa misingi ya Rushwa.
ü -Bei ya mbolea
inayonunuliwa kwa jumla ni kubwa kuliko bei ya rejareja.
ü- Kwenye soko kuna
madaraja 72 ya tumbaku ambapo tumbaku hiyo hiyo ikifika kiwandani Morogoro kuna
kitu kinaitwa inhouse grading inayotoa madaraja zaida ya 100.
No comments:
Post a Comment