Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Thursday, April 7, 2016

KATA YA BUKENE YAKUSUDIA KUMALIZA UPUNGUFU WA MADAWATI



Na Lucas Raphael,Nzega

Kata  ya Bukene wilaya ya Nzega mkoani Tabora imekusudia kumaliza tatizo la madawati katika shule za msingi na sekandari katika katani humo  kwa kuchonga madawati 500 nyenye thamani ya shilingi milioni 50.
 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mtendaji wa kata hiyo Daniel Kapama amesema kwamba kusudio hilo lilifikiwa kwenye kamati ya maendeleo ya kata kwa kuwashirikisha na wananchi wenyewe.

Amesema kwa kila mjumbe wa kamati hiyo hatachangia dawati moja na diwani wa kata hiyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya maendeleo hatachingia madawati  mawili.

Kapama amebainisha kuwa  kamati hiyo ilipendekeza kumuona afisa maliasilia ili kutoa kibali cha kuchana mbao kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo la madawati kabla ya Juni 30 mwaka huu.

Amesema kwamba madawati hayo yatasaidia kuondoa tatizo la kukaa chini ambalo limeongezeka baada ya kuandikishwa watoto 680 kuanza darasa la kwanza na wale wa awali ni watoto 425.

Kapama amesema  kutokana na idadi hiyo ya wanafunzi imepelekea kuongezeka kiwepo kwa upungufu wa madawati kwa baadhi ya shule katika kata hiyo.

Aidha Diwani wa kata hiyo Omary shabani Omary amesema katika maazimio yao pia wamedhamiria kujenga madarasa 4 ya shule ya msingi Bukene na jengo la utawala shule ya sekondari Bukene.
  
Amesema kwamba pia wamepanga kukamilisha ujenzi wa nyumba ya sekondari Bukene ambapo kila mjumbe wa kamati ya maendeleo ya kata atachangia mfuko  moja wa saruji na wananchi  watangia kiasi cha shilingi 4,100/=.

Omary ameeleza kwamba yeye diwani atachangia mifuko miwili ya saruji  na wafanyabiashara wataungana wawili wawili kwa ajili ya kuchangia mfuko moja wa saruji .



Sunday, April 3, 2016

YUSUPH KITUMBO, FATE REMTULLA WAFUNGIWA MAISHA KUSHIRIKI SOKA



YUSUPH KITUMBO

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili, Jerome Msemwa leo imetoa maamuzi ya shauri la upangaji wa matokeo ya kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League).
 
Akisoma hukumu hiyo baada ya kumaliza kuwahoji viongozi wa vilabu na wenyeviti wa vya vyama vya mpira wa miguu vya mikoa jana, Wakili Msemwa amesema adhabu hizo zimetolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF, na nafasi ya kukata rufaa kwa wahusika juu ya maaamuzi hayo ziko wazi.

Klabu za Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zimekutwa na hatia ya upangaji wa matokeo na kupewa adhabu ya kushushwa daraja mpaka ligi daraja la pili (SDL) msimu ujao.

Upande wa klabu ya JKT Kanembwa FC ya mkoani Kigoma, imeshushwa daraja mpaka kwenye ngazi ya ligi ya mkoa (RCL), baada ya kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi lake, Kundi C.

Kamati ya Nidhamu imewafungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu mwamuzi wa mchezo kati ya JKT Kanembwa FC v Geita Gold, Saleh Mang’ola na kamisaa wa mchezo huo Moshi Juma baada ya kukutwa na hatia ya upagaji matokeo.

Aidha kamati pia imemkuta na hatia kocha msaidizi wa klabu ya Geita Gold, Choke Abeid na kumfungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu.

Magolikipa Mohamed Mohamed wa JKT Kanembwa na Dennis Richard wa Geita Gold wamefungiwa miaka 10 kutojihusisha na mpira wa miguu sambamba na kulipa faini ya shilingi milioni kumi (10,000,000) kila mmoja.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita (GEREFA), Salum Kurunge, Mwenyekiti wa klabu ya Geita Gold, Cosntantine Moladi na Katibu wa klabu ya JKT Kanembwa Basil Matei wameachiwa huru na Kamati ya Nidhamu baada ya kutokutwa na hatia katika shauri hilo.

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Yusuph Kitumbo, Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Fateh Remtullah, Mwenyekiti wa klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita na kocha msaidizi wa Polisi Tabora, Bernad Fabian wamefungiwa maisha kutojihusisha na mpira wa miguu.

Mwamuzi wa mchezo kati ya Polisi Tabora v JKT Oljoro, Masoud Mkelemi na mwamuzi wa akiba, Fedian Machunde wamefungiwa kwa muda wa miaka kumi kutojihusisha na mpira wa miguu, na kutozwa faini ya shilingi milioni (10,000,000) kumi kila mmoja.

Katibu wa klabu ya Polisi Tabora, Alex Kataya, Katibu wa klabu ya JKT Oljoro, Hussein Nalinja, mtunza vifaa wa klabu ya Polisi Tabora, Boniface Komba, na Meneja wa timu ya  Polisi Tabora, Mrisho Seleman, wameachiwa huru na Kamati ya Nidhamu ya baada ya kutokutwa na hatia.

Kutokana na maamuzi hayo ya Kamati ya Nidhamu ya TFF, Kamati husika zitakaa kupitia Kanuni na kutangaza timu itakayopanda Ligi Kuu (VPL) msimu ujao na timu zitakazopanda Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes) msimu ujao.

COASTAL UNION YAZIDI KUTOTA, YANGA YABEBWA KWA VISINGIZIO


MATOKEO YA VPL

JUMAMOSI 2 APRIL,2016
1.
Mbeya City
4-0
Coastal Union
2.
Mwadui
1-2
Mtibwa Sugar
JUMAPILI 3 APRIL,2016
1.
Young African
V
Kagera Sugar
2.
V
3.
V
4.
V
5.
v

YANGA YABEBWA KWA VISINGIZIO

Siasa za Soka la Bongo kila kukicha zinachukua sura mpya baada ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF kukubali kuisogeza mbele mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar iliyopangwa kuchezwe Jumatano tarehe 6 April,2016 na badala yake itachezwa tarehe 16 April,2016 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya klabu ya Yanga kulalamika kupangiwa mechi tatu ndani ya wiki moja kabla ya kuvaana na Al Ahly ya Misri Jumamosi ijayo ya terehe 9 April,2016 kwenye kinyang’anyiro cha ligi ya Mabingwa Afrika.

Swali la kujiuliza Madai hayo ya Klabu ya Yanga yanamsingi wowote katika soka la kisasa linalotawaliwa na uwekezaji wa rasilimali fedha,vifaa,watu na maarifa.

Kama kweli tunataka kuimarisha Soka la Bongo inatupasa kuacha visingizio, hoja na mitazamo ya kisiasa mahali tunapotakiwa kuonyesha vitendo na uwezo zaidi.

Chukua mfano huu Jumamosi April 2,2016 Barcelona na Real Madrid zimecheza mechi yao ya ligi inayojulikana kama “El Clasico” ambapo Real Madrid iliishinda Barcelona kwa magoli 2 kwa 1.

Kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Jumanne April 5,2016 Barcelona itakuwa kwenye uwanja wa nyumbani Camp Nou kuikaribisha Atletico Madrid ikiwa ni hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Aidha Jumatano April 6,2016 Real Madrid itakuwa ugenini kwenye uwanja wa “Volkswagen Arena” kuivaa VfL Wolfsburg kwenye UEFA Champions League.

Timu hizo vigogo kwenye ligi kuu ya Hispania zitashuka Dimbani kwa mara nyingine Jumamosi ya tarehe 9 April,2016 ambapo Barcelona itasafiri hadi kwenye uwanja wa Anoeta kucheza na Real Sociedad, wakati Real Madrid itakuwa nyumbani Santiago Bernabeu wakiikaribisha timu ya Eibar.

Hii inamaana kuwa timu hizo za Barcelona na Real Madrid zinashuka dimbani mara tatu ndani ya wiki moja na  hatujasikia zikilalamikia ratiba au kupewa muda wa kujiandaa na UEFA Champions League.

Utaratibu huo makini uliowekwa na watu wenye mikakati na mtazamo wenye kuzingatia weledi wa taaluma, biashara na uwekezaji wa hali ya juu unaonekana dhahiri kwenye ligi za Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Italia na nchi nyingine zilizopiga hatua kisoka.

Kama utaratibu huo unawezekana mahali pengine duniani na timu zinafanya vizuri ni kipi kinashindikana kwa Yanga ambayo inanolewa na  kocha wa kigeni muholanzi Hans van der Pluijm.

Yanga pia imesheheni wachezaji wa kimataifa akiwemo Vincent Bossou (Togo) , Donald Ngoma, Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima (Rwanda), Andrey Coutinho (Brazil) na Amis Tambwe (Burundi).

Kwangu mimi naona tunayosafari ndefu ya kufikia mafanikio ya KWELI katika mchezo wa soka wenye mashabiki wengi, fedha nyingi na uwekezaji mkubwa kama timu zetu zitaendelea na siasa za kubebwa na kuonewa huruma.

Friday, April 1, 2016

RADI YAUA MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA



Na Paul Christian, Tabora.

Mwanafunzi wa kike wa darasa la kwanza shule ya msingi Kakurungu kata ya Milambo Itobo wilayani Nzega Asia Paulo amefariki dunia baada ya kupigwa na radi.

Akizungumza na waandishi wa habari mtendaji wa kata ya Milambo Itobo Raphael Bundala amesema tukio hilo limetokea Alhamis mchana katika familia ya Ngelengi Makala katika kitongoji cha Mtakuja kijiji cha Kakurungu katani humo.

Amesema wakati wa majira hayo ya mchana ilinyesha mvua ya wastani iliyoambatana na radi ilipiga kwenye jiko la familia  hiyo na kusababisha kifo cha mwanafunzi huyo na kujeruhi watu wengine wanne. 

Raphael amewataja watu waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Hadija Juma mwenye umri wa miaka 40 amejeruhiwa ubavuni na sehemu ya paja, Sophia Ngelengi mwenye miaka 25 amejeruhiwa mbavuni,Salima Rashid mwenye miaka 21 amejeruhiwa kwenye paji la uso na mtoto wa miaka 6 Abdalla Ramadhan alipata majeraha miguuni.

Mtendaji huyo amefafanua kuwa majeruhi wote walitibiwa katika zahanati ya Kakurungu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.