Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Tuesday, March 1, 2016

LIVERPOOL YAICHAKAZA MAN CITY, ARSENAL YAANGUKIA PUA, MAN UNITED YAOKOTA POINT 3, TOTTENHAM YATOLEWA NISHAI


MATOKEO NA MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA EPL

Jumanne 01 Machi, 2016
1.
Aston Villa
- Rudy Gestede (79)
1-3

Everton
Ramiro Funes Mori (5)
Aaron Lennon (30)
Romelu Lukaku (60)
2.
Bournemouth

- Steve Cook (31)
Benik Afobe (79)
2-0

Southampton
3.
Sunderland

- Dame N'Doye (36)
Fabio Borini (90)
2-2

Crystal Palace
Connor Wickham (61)
Connor Wickham (67)
4.
Leicester City

- Daniel Drinkwater (30)
Andy King (46)
2-2

West Bromwich Albion
Salomon Rondon (11)
Craig Gardner (50)
5
Norwich City

- Nathan Redmond (68)
1-2

Chelsea
Robert  Nascimento (1)
Diego Da Silva Costa (46)
Jumatano 02 Machi,2016
1.
Stoke City
Xherdan Shaqiri (80)
1-0
Newcastle United
2.
West Ham United
-Michail Antonio (7)
1-0
Tottenham Hotspur
3.
Arsenal
Joel Campbell (15)
1-2
Swansea City
Wayne Routledge (32)
Ashley Williams (74)
4.
Manchester United
Juan Mata (83)
1-0
Watford
5.
Liverpool
Adam Lallana (34)
James Milner (41)
Roberto Firmino Barbosa de Oliveira (57)
3-0
Manchester City

MSIMAMO 


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Leicester City
28
16
9
3
51
31
20
57
2
Tottenham Hotspur
28
15
9
4
49
22
27
54
3
Arsenal
28
15
6
7
44
28
16
51
4
Manchester City
27
14
5
8
48
31
17
47
5
Manchester United
28
13
8
7
37
26
11
47
6
West Ham United
28
12
10
6
42
31
11
46
7
Stoke City
28
12
6
10
30
33
-3
42
8
Liverpool
27
11
8
8
41
36
5
41
9
Southampton
28
11
7
10
35
28
7
40
10
Chelsea
28
10
9
9
42
38
4
39
11
Everton
27
9
11
7
49
36
13
38
12
Watford
28
10
7
11
29
29
0
37
13
West Bromwich Albion
28
9
9
10
29
36
-7
36
14
Crystal Palace
28
9
6
13
31
37
-6
33
15
Bournemouth
28
8
8
12
32
44
-12
32
16
Swansea City
28
7
9
12
27
37
-10
30
17
Sunderland
28
6
6
16
34
53
-19
24
18
Norwich City
28
6
6
16
31
53
-22
24
19
Newcastle United
27
6
6
15
27
50
-23
24
20
Aston Villa
28
3
7
18
22
51
-29
16

WAUGUZI SITA WASIMAMISHWA KAZI HOSPITALI YA TEMEKE, DAR ES SALAAM



Dkt. KIGWANGALA
Na Cathrine Sungura, Dar es Salaam.

Wauguzi sita wa wodi ya akinamama wajawazito wa hospitali  ya rufaa ya Temeke,wamesimamishwa kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yao wakati wa kuwahudumia akinamama wanaofika kujifungua kwenye hospitali hiyo.

 Hatua hiyo imefikiwa kwenye ziara iliyofanywa hospitalini hapo na naibu waziri wa wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangwala.

Aidha,wauguzi hao wanatakiwa kifikishwa kwenye baraza la wauguzi na wakunga kwa kukosa uadilifu wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Waliosimamishwa kazi ni pamoja na Beatrice Temba, Marian Mohamed, Hadija Salum, Elizabeth Mwilawa, Agnes Mwapashe na Merion Said.

Hata hivyo Dkt. Kigwangwala ametoa siku 30 kwa manispaa ya Temeke kukamilisha chumba cha upasuaji cha akina mama wajawazito,miezi sita kwa vyumba viwili vya upasuaji  kuvifanyia ukarabati mkubwa na kuwa katika ubora unaotakiwa,miezi mitatu kwa  chumba  cha watoto wachanga kwa kuongeza vitanda 25 hadi 30  kutoka vitanda 9 vya awali ili kuepusha magonjwa ya kuambukiza.

KIKWETE APONGEZWA KUTEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA WA CHANJO DUNIANI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA



TAARIFA KWA UMMA KUFUATIA KUTEULIWA KWA MHESHIMIWA RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUWA BALOZI WA HESHIMA WA CHANJO DUNIANI KUPITIA SHIRIKA LA GAVI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa furaha uteuzi uliofanywa na Shirika la Global Alliance for Vaccines and Immunizations (GAVI) kwa  kumteua Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais  Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Balozi wa Heshima wa Chanjo Duniani. Kwa niaba ya Serikali, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa niaba yangu binafsi napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi huu.

Ndugu wananchi, 

Kama mlivyosikia kwenye vyombo vya habari  Rais wetu mstaafu wa awamu ya nne (4) Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuwa BALOZI WA HESHIMA WA CHANJO DUNIANI kupitia shirikia laGlobal  Alliance for Vaccines  and  Immunizations (GAVI) mnamo tarehe 31Januari,2016 nchini Ethiopia.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuchukua fursa hiikuungana na shirika la GAVI pamoja na wananchi wote wa Tanzaniakumpongeza Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi huo. Kuteuliwa  kwake kuwa Balozi wa heshima kwenye masuala ya chanjo, kuna maana ya kuwa,atakuwa mhamasishaji wa  wakuu wote wa nchi  za Afrika na dunia kwa ujumla kuhakikisha  wanaweka kipaumbele katika  upatikanaji wa huduma za afya hususan masuala ya chanjo.

Katika muda wote wa uongozi wake Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alitoa kipaumbele  katika  masuala ya afya ya uzazi  na  mtoto  likiwemo suala la chanjo   na  kuhakikisha wanawake na watoto  wanapata huduma ipasavyo.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Watanzania wote tumefarijika sana kwa uteuzi huo, kwani pamoja na juhudi hizo, amekuwa  ni Mwenyekiti mwenza wa Jopo la watu mashuhuri la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  juu ya uboreshaji wa malengo ya  Maendeleo  endelevu.(Sustainable Development Goals)

Aidha,Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alishiriki katika mkutano mkubwa wa GAVI uliofanyika mnamo tarehe 26 hadi 27Januari  2015 nchini Ujerumani na kueleza dhamira yake na ya nchi kwa ujumla katika kushiriki kikamilifu kupunguza kiwango kikubwa cha maradhi na vifo vitokanavyo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Tanzania iliweza kuongeza kiwango cha  utoaji wa huduma za chanjo hadi  kufikia  wastani wa zaidi ya asilimia 95 ikiwa ni zaidi ya lengo la Kimataifa la  asilimia  90.Tunaami kuwa mafanikio haya yamechangia Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kupewa heshima hiyo.

Historia inaonyesha kuwa kwenye miaka ya sabini watoto wengi walipoteza maisha yao kutokana na magonjwa yanayozuilika  kwa chanjo.Wengi wetu ni mashahidi wa milipuko na vifo vilivyotokana na ugonjwa wa surua kipindi hicho. Wodi nyingi katika Hospitali zetu zilitengwa na zilijaa watoto waliougua surua na ugonjwa wa pepo punda.  Aidha, watoto wengi  walibakia na ulemavu wa viungo, ulemavu wa kutoona, ulemavu wa kutosikia,  na mtindio wa ubongo kutokana na athari za magonjwa ya polio na  surua.

Juhudi za Serikali katika kukabiliana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo zimeleta mafanikio makubwa. Kwa mfano, magonjwa ya ndui na pepopunda kwa watoto wachanga yametoweka,pia tumeshuhudia wodi za surua zikifungwa, na vifo vitokanavyo na surua kupungua kwa kiasi kikubwa.Aidha Tanzania imekwisha thibitishwa kuwa ni miongoni mwa nchi zilizotokomeza ugonjwa wa Polio duniani. Mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za Serikali  kuwekeza katika chanjo.

Imethibitika kuwa chanjo ni mkakati muafaka katika kutokomeza magonjwa  na kupunguza vifo vya watoto, hivyo kupunguza gharama kubwa ambazo familia zetu na Taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu maradhi yatokanayo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Rejea za kitaaluma zimethibitisha kuwa chanjo huzuia takribani vifo Milioni 2 hadi 3 kila mwaka kutokana na maradhi yanayozuilika  kwa chanjo duniani. Nchini Tanzania,  mwaka 2004, vifo vya watoto chini ya miaka mitano vilikuwa 112 kati ya vizazi hai 1,000 na viliendelea kupungua hadi vifo 81 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2010.

Mojawapo ya mikakati ya Mheshimiwa  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika kipindi chake cha uongozi ilikuwa ni kufikia malengo ya maendeleo ya Milenia. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa (UN Inter Agency Report for child mortality estimates), Tanzania ilifanikiwa kufikia lengo la Millenia namba 4 la kupunguza vifo vya watoto walio na umri chini ya miaka 5 kutoka vifo 81 hadi vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2013.

Tunafahamu kuwa Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ana kazi kubwa mbele yake ya kuhakikisha nchi zote za Afrika na Dunia kwa ujumla zinafikia kiwango cha wastani wa asilimia 90 wa chanjo kwani, hadi sasa,  bado kuna nchi ambazo bado zina kiwango cha wastani wa asilimia 50.

Ni faraja yetu kubwa  kuwa Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ataendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha  upatikanaji wa huduma za chanjo barani  Afrika na dunia kwa ujumla na hivyo kuokoa maisha ya watoto. 
 
Tunamtakia mafanikio mema katika utekelezaji wa majukumu hayo makubwa kidunia,na kumuahidi ushirikiano wetu.

Imetolewa na ;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
1.3.2016

WATOTO YATIMA NA WA MAZINGIRA DUNI WAISHUKURU SERIKALI YA JAPANI


PICHA KUTOKA MAKTABA
Na Halima Ikunji,Uyui.


Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira duni 159 katika kata za Ilolangulu na Isila wilaya ya Uyui mkoani Tabora,wameishukuru Serikali ya Japan kwa kuwasaidia kupata majengo mawili ya kituo cha kulelea watoto hao.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika sherehe fupi ya kukabidhi mradi wa ujenzi wa kituo hicho kilichojengwa kijiji cha mbola kilichopo kwenye mradi wa vijiji vya milenia, wamesema mradi  huo kupitia ufadhili wa serikali ya Japan umewanufaika katika sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya maji, elimu na afya.

Watoto hao wamebainisha kuwa wazazi wao walifariki kwa magonjwa mbalimbali na kuwaacha wakiwa wadogo ambapo  walezi wao katika familia hawakuwa na uwezo wa kuwatunza hali iliyowasababisha kuwa  ombaomba,vibaka na wengine kufanya ukahaba ili wajipatie chakula.

Awali katika sherehe hizo mratibu wa mradi wa vijiji vya milenia Dkt, Grerson Nyadzi amesema kuwa kituo hicho kimejengwa kwa muda wa miezi 10 kuanzia mwezi Mei mwaka uliopita na umegharimu zaidi ya Tsh. Mil 176.

Nyadzi amebainisha kuwa licha ya kukamilika kwa majengo hayo mawili bado kunahitajika  vitanda, magodoro, vyandarua,  jiko la kupikia chakula na vifaa vya ofisini hivyo ameiomba Serikali ya Tanzania iweze kuunga mkono juhudi hizo.

Mratibu huyo amesema kuwa katika ujenzi huo jamii ilishirikishwa kwa kuchangia nguvu kazi yenye thamani ya Tsh. Mil. 12.9 ambapo wafadhili walichangia Tsh. Mil. 163,601,448 sawa na dola za kimarekani 91,4996. 

Nae Balozi mdogo wa Japan, Hiloyuki Kubota katika hotuba yake amesema  kuwa kituo hicho cha watoto hao kitakuwa na uwezo wa kupokea watoto wengine 96 ambao wanaishi katika mazingira magumu na wasio jiweza kiuchumi.

Balozi Kubota amebainisha kuwa Serikali ya Japan inalenga kusaidia maeneo hayo katika Jamii, kwani anaimani kwamba kituo hicho kitasaidia watoto hao kwa kuwapa mazingira bora na nafasi za kutimiza ndoto zao.

Aidha  Balozi huyo ameiomba halmashauri ya wilaya ya Uyui kutenga bajeti kwa ajili kwa ajili ya kuendesha wa kituo hicho.