Na,Thomas Murugwa, Tabora.
Serikali ya
awamu ya Tano imetakiwa za kunusuru maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi
vinavyotokana na ugonjwa wa saratani ya ngozi.
Uchunguzi
uliofanywa na blog hii umebaini kuwa vifo 10 vya watu wenye ulemavu wa
ngozi vimetokea kati ya Januari na Mei 2016 mkoani Tabora
kutokana na ugonjwa huo kwa kukosa mafuta maalumu yanayosaidia kupunguza
mionzi ya jua kuifikia ngozi ya watu hao.
Katibu
wa chama cha Maalbino mkoani Tabora Ramadhani Nassoro amesema saratani ya ngozi imesababisha vifo
hivyo na hiyo imekuwa ni changamoto kwao
kwa kuwa inachangia kufupisha maisha ya watu
wenye ulemavu wa ngozi.
Amesema
kuwa watu wanye ulemavu wa ngozi wengi wao maisha yao hayazidi miaka (40) kwa
kuwa wanakabiliwa na hatari ya saratani ya ngozi ambayo inatokana na kufikiwa
na mionzi ya jua moja kwa moja.
Nassoro
amebainisha kuwa albino wanakutana na mionzi ya jua kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo kufanya kazi za kujipatia kipato kama kilimo,
uchungaji,ujenzi na nyingine katika maeneo ya wazi.
Naye
Juma Mosha katibu wa chama cha Albino wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameiomba
serikali ichukue jukumu la kuwapatia mafuta hayo maalumu kupitia hospitali na vituo vya afya ili kuwanusuru na
saratani ya ngozi ambayo inakatisha maisha yao kwa kiwango kikubwa.
Katibu
huyo amebainisha kuwa mafuta hayo yanagharama kubwa hali ambayo albino wengi
hawawezi kumudu na kwamba wakati umefika kwa serikali kuwasaidia kama ambavyo
imeamua kufanya hivyo kwa wazee.
No comments:
Post a Comment